Tangazo

January 28, 2015

Airtel yatoa msaada wa vitabu katika shule ya Secondary Nanja - Monduli Arusha

Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha wakishuhudia kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde  na kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nanja Yona Lukas.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde  akipitia kitabu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

· Chini ya mpango wake wa shule yetu, shule za sekondari manyara, Moshi na Tanga kupokea msaada huo mwenzi huu

Wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Nanja wamepokea msaada wa vitabu kutoka Airtel, Msaada utakaoweza kuchangia katika kutatua tatizo la uhaba wa vitabu shule ni hapo.

Akitoa taarifa ya shule , Mkuu wa shule ya sekondari ya Nanja Bwana Yona luka alisema” shule yetu ina jumla ya wanafunzi 549 na walimu 32,  matokeo ya shule ya kidato cha nne yanakuwa kila mwaka ufaulu wa asilimia 71% pamoja na kukua kwa kiwango cha ufaulu bado shule inachangamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vitabu na walimu.  Kwa sasa uwiano  wa vitabu vya sayansi ni kitabu 1 kwa wanafunzi 5 wakati kwa vitabu vya sayansi ya jamii uwiano ni kitabu 1 wanafunzi 30. Tunafurahi sana kupokea vitabu hivi toka Airtel kwani msaada huu umekuja kwa wakati muafaka”

Akiongea wakati halfa hiyo fupi ya kukabithi vitabu , Afisa Elimu wa shule za sekondari halmashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya alisema” napenda kuwashukuru sana Airtel kwa kufikisha msaada huu wa vitabu kwa sekondari hii ya Naja , vitabu hivi vya sayansi havitachangia kuongeza kiwango cha ufaulu tu bali vitawahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi. 

Natoa wito kwa walimu kuwapatia wanafunzi vitabu hivi wavisoma ili kuwajengea wanafunzi hawa tabia ya kusoma vitabu. Nawahasa wanafunzi kuvitunza vitabu ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi shuleni hapa.

Aliongeza kwa kusema” shule imeweza kujenga maktaba lakini tunayochangamoto ya uhaba wa vifaa vya maktaba , nachukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kutusaidia kwa kuchangia vifaa vya mahabara na kuwezesha masomo ya sayansi ya vitendo”

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja wa kanda ya kaskazini Brighton Majwala alisema”wote tunatambua tatizo la uhaba wa vitabu katika shule za sekondari ambapo hali halisi haiendani namahitaji, uwiano wa kitabu 1 ni kwa wanafunzi 10. Kwa kuliona hilo Airtel tumejikita na kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunatutua changamoto hii na kuongeza kiwango cha ubora wa elimu nchini.  Natoa wito kwa wanafunzi wa Nyala kuzitumia vitabu hivi vizuri na kuboresha kiwango cha ufaulu.

Kwa upande wa wanafunzi wameishukuru Airtel kwa kuboresha elimu na kusema vitabu hivi vitawasaidia kuongeza ujuzi katika masomo ya sayansi na kufanya vizuri zaidi.

Halfa ya kukabithi vitabu katika shule ya sekondari Nanja ilimalizika kwa zoezi la kupanda miti ambapo walimu, wanafunzi na Airtel walishiriki katika kuboresha mazingira ya shule.

Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu mpaka sasa imezifikia shule zaidi ya 1300 nchini, shule nyingine katika kanda ya kaskazini zitakazofaidika na vitabu hivi ni pamoja na  Manyara, Moshi na Tanga na shule nyingine katika maeneo mbalimbali ya nchi nazo zitaendelea kupata msaada huu wa vitabu.

No comments: