Tangazo

January 9, 2015

FAINALI YA SOKA YA UDSM AIRTEL UNI255 KURUDIWA JUMAMOSI HIINa: Mwandishi Wetu

Fainali ya Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) inayojulikana kama Airtel UNI255 iliyoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuo kikuu  itarudiwa siku ya jumamosi ya tarehe 10/1/2015 kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) baada ya Fainali hiyo kushindwa kumalizika  na kukosa  mshindi  kutokana na Kiza kilichoingia na kuleta mkanganyiko wa nani anastahili kuwa Bingwa katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Fainali hiyo ambayo ilivikutanisha vyuo vya Sayansi ya Jamii (College of Social Science) na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (College of Engineering and Technology) hadi dakika tisini(90) za mchezo zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Akizungumzia marudio ya fainali hiyo, waziri wa michezo wa Serikali ya wanafunzi  katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, STANLRY JULIUS  alisema kuwa michezo hiyo ilileta changamaoto kubwa sana katika chuo hicho na kitendo cha kutopata mshindi kilitokana na kuchelewa kuanza kwa fainali hiyo ambayo hata hivyo baada ya Uongozi wa chuo kukaa na kutathmini waliamua mechi hiyo irudiwe ili kupata mshindi wa kwanza na wa pili kwa kuwa timu hizo zitatakiwa kuungana na timu zingine za jiji la Dar es salaam katika ligi ya kutafuta chuo bora katika mchezo wa mpira wa miguu.

“kikubwa tu ni kwamba tunaishukuru kampuni ya simu za mkononi AIRTEL kupitia mpamgo wake wa UNI255 kwa kusapoti michezo hii ya vyuo, bila shaka Tanzania kupitia shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania(TFF) linaweza pia kunufaika na michezo hii ya vyuo kwa kupata wacheza watakaoisaidia Nchi kwenye timu ya Taifa”alisema STANLRY JULIUS

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa serikali ya wanafunzi, Mchezo huo wa fainali utafanyika kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam mapema kuanzia saa tatu kamili asubuhi na unatazamiwa kumalizika saa tano na baada ya kumalizika kwa mchezo huo hafla ya kukabidhi zawadi itafanyika kwenye tawi la chuo hicho Mabibo Cumpas na amesisitiza kwamba suala la usafiri kwa wanafunzi ni bure na usafiri utakuwa mwingi wakati wote kwenda Mabibo na kurudi chuo Kikuu kuanzia asubuhi hadi jioni. 

Naye Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa kutokana na kukosa mshindi kwenye mchezo wa fainali wao wakiwa ndo wadhamini wakuu walilitazama kwa namna ya pekee hivyo wameamua kuongeza bajeti ingine ili kuhakikisha kwamba fainali hiyo inapata mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.

Michezo inaleta afya na ndiyo maana tumeamua kutumia gharama nyingine tena ili kuunga mkonpo jitiada za chuo kikuu cha UDSM kufanikisha michezo hii ya Vyuo,”alisema Jackson Mbando

Aidha katika kilele cha marudio ya fainali hiyo Airtel imeandaa burudani mbali mbali ikiwemo mbio za Piki piki, Mashindano ya Vipaji vya kuimba, kucheza, pamoja na wasanii akiwemo Roma Mkatoliki, Shilole anaetamba na wimbo wake mpya wa Malele, ney wa mitego ambapo hawa wataongozwa na DJ maarufu jijini Dj Zero

No comments: