Tangazo

January 26, 2015

KINANA ASHIRIKI UPANDAJI WA ZAO LA MWANI KUSINI UNGUJA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda zao la mwani katika Kijiji cha Kibigija, Jambiani, Wilaya ya Kusini Unguja, Zanzibar leo, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM pamoja na wakulima wakiondoka baada kushiriki kupanda mwani
 Komredi Kinana akilakiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi, Haroun Ali Selemani alipowasili Kijiji cha Pete, Wilaya ya Kusini Unguja.
 Komredi Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Samia Suluhu Rashid alipowasili katika Kijiji cha Pete kusomewa taarifa ya chama na Serikali.
 Kinana na Mbunge wa Jimbo la Muyuni, Mahadhi Juma Mahadhi wakitumia matoroli kubeba udongo wa kujengea jengo la CCM Jimbo la Muyuni
Baadhi ya watalii wakipiga picha msafara wa Kinana eneo la Muyuni
 Kinana akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa Wilaya ya Kusini, Haji Abdallah Haji alipomtembelea nyumbani kwake Kibigija
                              Zao la mwani likiwa limevunwa
 Wanahabari walio kwenye msafara wa Kinana wakipita kwenye madimbwi wakitoka kufanya caverage wakati Kinana akishiriki kupanda mwani katika Kijiji cha Kibigija, Jambiani, Kusini Unguja
Kinana akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Ukumbi wa CCM tawi la Mtende
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kizimkazi Mkunguni uliohutubiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu, Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye.
 Komredi Kinana akirekodi matukio mbalimbali kwenye mkutano huo
 Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Samia Suluhu akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuipigia kura ya ndiyo KKatiba inayopendekezwa Aprili 30 mwaka huu.
 Moja ya vionjo katika mkutano huo
 Baadhi ya wananchi wakinyoosha juu mikono kukubali kuipigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano huo, ambapo alisema kuwa viongozi wa Umoja wa Katiba ya wananchi wameanza kutapatapa kwa kutangaza kususia upigaji kura wa Katiba inayopendekezwa.
 Shemu ya umati wa wananchi wakiwa katika mkutano unaohutubiwa na Komredi Kinana kwenye Uwanja wa Kizimkazi Mkunguni
 Kinana akikabidhi moja kati ya majiko ya gesi kwa mmoja wa madiwani wa Jimbo la Makunduchi kwa ajili ya kuwafundishia akinana waweze kutumia majiko hayo ili kutunza mazingira kwa kuacha kukata kuni.
 Kinana akiwakabidhi vijana kasha lenye jezi na mipira kwa ajili ya timu 18 ili kuendeleza michezo jimboni humo. vifaa hivyo vyote vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Samia Suluhu na Mwakilishi wa jimbo hilo, Haroun Ali Selemani.
Kinana akikabidhi pikipiki nne kwa ajili ya kikundi cha kukagua uhifadhi wa mazingira katika jimbo hilo.

No comments: