Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na
waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri jijini Dar es Salaam leo.
**********
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa
wake wa uwaziri hii leo.
Prof.
Muhongo ametangaza uamuzi huo asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi wa
habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini.
Akitangaza
uamuzi huo Prof. Muhongo amesema ameamua kuachia wadhifa huo ili kupisha nchi
ijadili na kufanya mambo muhimu ya maendeleo badala ya kuendelea kujadili
masuala ya Escrow.
"Wananchi
wamechoka, na hata mimi mwenyewe nimechoka kila kukicha watu wanajadili ESCROW,
hivyo anajiuzulu ili watu wafanye kazi na kuleta maendeleo," alisema prof
Muhongo.
Aidha
amesema sakata yeye anaendelea kusisitiza na kusimamia msimamo wake kuwa
hahusiki kwa namna yeyote ile katika uchukuaji wa fedha za akaunti ya Escrow
kama inavyodaiwa na watu.
Waziri
huyo amejiuzulu ikiwa ni baada ya kuitumikia wizara hiyo kwa kipindi cha miaka
miwili na nusu tu, huku akiwa amefanya jitahada kubwa kuhakikisha wananchi
vijijini wanapatiwa umeme kwa gharama nafuu.
Muhongo
amesema ni wakati mzuri sasa kuviachia vyombo vya dola hasa Mahakama kujadili
suala la Escrow na sio watu wengine mitaani.
No comments:
Post a Comment