Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane
Matinde akijadiliana jambo na waandishi wa habari kuhusu promosheni ya Airtel
yatosha zaidi wakati wa mkutano wa kuitambulisha promosheni hiyo kwa wakazi wa
mkoa wa Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kufanya
droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi siku ya kesho Ijumaa
tarahe 13 februari 2015 ambapo washindi 7 wa gari aina ya Toyota IST
watapatikana na kutangazwa.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa
kuitambulisha promosheni ya Airtel yatosha zaidi kwa wakazi wa Mkoa wa
Dodoma, uliofanyika Dodoma Hoteli, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane
Matinde alisema” kama ilivyo kawaida tunazunguka katika mikoa mbalimbali kutoa
elimu juu ya huduma na bidhaa zetu pamoja na kuitambulisha promosheni hii
ya Airtel Yatosha Zaidi tuliyoizindua hivi karibuni inayo wapa wateja wetu na
watumiaji wa vifurushi vya Airtel yatosha nafasi ya kujishindia gari aina ya
Toyota IST kila siku.
Mpaka sasa tunao washindi watatu waliopatikana na Tayari
wawili wamekabithiwa magari yao akiwemo Mwajuma Churian Mkazi wa Dar es saalam
aliyekabithiwa gari lake siku ya Jumanne na leo Alhamisi tunakabithi gari kwa
mwalimu mstaafu mkazi wa Mtwara Bwana Namtapika Kilumba . Mshindi wa tatu
aliyetangazwa ni Bwana Ramadhani Dilunga ambaye ni Mkulima anatokea mkoa
wa Pwani.
Nachukua fulsa hii kuwajulisha watanzania kuwa droo ya wiki
ya pili ya promosheni hii inategemea kufanyika kesho siku ya Ijumaa ambapo
washindi saba watapatikana na kutangazwa, tunaomba wateja wakae karibu na simu
zao na watapigiwa simu za kutangiziwa ushindi huo toka namba 0684291105
ambapo Watanzania na wateja wetu 7 kesho wataondoka na Toyota IST.”
Napenda kutoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi
hivi vya Airtel yatosha kufanya hivyo kwa kupiga *149*99# , au kununua vocha za
Airtel yatosha au kununua vifurushi hivi kupitia huduma ya Airtel Money
sasa. Kila mtanzania na mtumiaji wa huduma ya Airtel yatosha ataingia
kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo ni wakati kwa wakazi wa
Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania kuchangamkia fulsa hii. Aliongeza Matinde.
Airtel Yatosha Zaidi ni promosheni iliyozinduliwa na kampuni
ya simu ya mkononi ya Airtel mwanzoni mwa mwezi wa pili mpaka sasa watanzania
wameendelea kubahatika kwa kujishindia magari aina yaToyota IST, promosheni hii
itadumu kwa muda wa miezi miwili.
No comments:
Post a Comment