Tangazo

May 25, 2015

KUMEKUCHA JIMBO LA ISMANI, LUKUVI APATA MPINZANI

 
 WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI
 
WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI

NA RAYMONDI MINJA IRINGA

MSOMI  wa Shahada ya uhandisi wa kilimo na mtaalamu  wa kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA), Mhandisi Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM  linaloshikiliwa na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Vangimembe Lukuvi
.

Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi,  Kayoyo alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.
 
Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani  hajafanya mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele  gurudumu la maendeleo katika nchi hii.
 
"Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na  ameweza kufanya mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali" Kayoyo.
 
Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi tarafa uya idodi  iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani

Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge,”Mimi ni mtumishi wa serekalina ninajua raratibu zote za utumishi serikali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu wa Isimani katika kujiletea maendeleo”

 Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha  lami kwa kwa kuwa  jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata uhuru wake

"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda kuona  wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu" alisema Kayoyo

Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo  kunafanya idadi ya wagombea kutoka chama  cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo,Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza huku kwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamoja makamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi

No comments: