Tangazo

May 16, 2015

NIMEPATA KUWA MBUNGE ILA SIKUFANYA KAMA FILIKUNJOMBE - KOLIMBA

 Aliyekuwa mbunge Ludewa kati ya mwaka 2002- 2005  Bw Stanile Kolimba  akieleza ubora  wa mbunge  wa  sasa wa Ludewa Deo Filikunjombe na  wabunge waliopita
mkazi  wa kijji  cha Lupanga akilia kwa furaha baada ya  mbnge wao Filikunjombe kuwasaidia kitanda cha  kujifungulia wakati awali walikuwa hawana

 mwenyekiti  wa  kijiji  cha Lupanga  akiwa amepiga magoti juu ya mezi  kumpongeza Filikunjombe  kwa kazi nzuri
 katibu mwenezi wa ccm mkoa  wa njombe Bw mgaya akicheza na msanii aliyevaa majani



mbunge  wa  ludewa  deo  filikunjombe wa  pili  kushoto  akisaidiana  na  wananchi  wake  kushusha bati na  saruji kwa ajili ya kijiji cha lupanga
wanafunzi  wa  shule ya msingi lupanga  wakitoa zawadi mbali mbali kwa mbunge filikunjombe baada ya kujitolea  kufanya ukarabati wa  shule yao
Filikunjombe akitazama vifaa mbali mbali  vya ujenzi alivyovitoa kijiji  cha Lupanga
wananchi  wakitoa  zawadi ya mbuzi kwa mbunge  wao
mbunge  filikunjombe akionyesha darubini aliyoitoa msaada  kijiji cha lupanga kwa ajili ya zahanati
mbunge filikunjombe akipongezwa kwa msaada wa  kitanda cha  kujifungulia  wajawazito
mbunge Filikunjombe akikabidhi jezi
wanahabari  joyce na deo nyoni wakifuatilia mkutano wa mbunge
katibu mwenezi wa ccm mkoa  wa Njombe Honolatus Mgaya  akizungumza na  wananchi wa Lupanga
diwani  wa  Lupanga  akifurahia jambo
Filikunjombe akiwashukuru wananchi wake
wananchi  wakimpongeza mbunge  wao kwa  misaada mbali mbali
wananchi  wakifurahi na mbunge  wao
mkazi  wa  Lupanga  akitembelea magoti kama sehemu ya ahsante kwa  mbunge
Filikunjombe akisalimiana na watoto wa  shule ya  Lupanga

Na  MatukiodaimaBlog , Ludewa

ALIYEKUWA mbunge wa sita toka nchi  ipate  uhuru katika   jimbo la Ludewa   Stanley Kolimba amempongeza mbunge  wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe kwa  utendaji kazi wake na  kuwa mbali  ya  kuwa amepata  kuwatumikia  wananchi  wa jimbo   hilo kwa nafasi ya   ubunge  ila hakuweza  kufanya mambo makubwa kama  yanayofanywa na mbunge  wa  sasa  katika   jimbo  hilo.

Kolimba  alitoa kauli  hiyo  jana  wakati akimshukuru  mbunge Filikunjombe kwa kusaidi  vifaa mbali mbali  vya ujenzi  vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 10 katika   kijiji  cha Lupanga kata ya  Lupanga  wilaya ya  Ludewa .

Alisema jimbo hilo  la Ludewa  limepata   kuwa na  wabunge saba  hadi  sasa  toka  nchi  ipate  uhuru   wake  mwaka  1961  ila kazi  kubwa  inayofanywa na mbunge  huyo  wa awamu ya saba Bw  Filikunjombe hakuna  mbunge  ambae  amepata  kuifanya na  kuwa  kuna haja ya  wananchi wa  wilaya ya  Ludewa na viongozi  kumpongeza  mbunge  huyo kwa utendaji kazi  na  uwakilishi  wa  wananchi  uliotukuka. 

"kweli  kwenye  ukweli  tuseme  kweli  mimi  bila shaka  mnanifahamu  vizuri  kuwa  mwaka  2001  nilikuwa mbunge  wa  jimbo  hili la Ludewa  na  kweli  kama  vitu  nilifanya   ikiwa ni pamoja na  kupeleka  umeme  Ludewa  mjini  na  kuna  siku katika  kuhamasisha maendeleo   nilipata  kukabidhi mbuzi mmoja  ila  lazima  niwe mkweli kasi  hii  ya Filikunjombe katika  kuwaletea maendeleo ni  kubwa  sana ukilinganisha na  sisi  wabunge  wote  tuliopita ...sio kama nampigia debe ila ndio ukweli wenyewe"

Hata   hivyo  Kolimba  ambae ni  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa  alisema   heshima  kubwa ya  wananchi  wa Ludewa kwa  sasa  imeanza kuonekana  kutokana na jitihada  kubwa zinazofanywa na mbunge  huyo na kuwa nguvu ya  chama tawala .

Katibu  mwenezi  wa CCM mkoa  wa Njombe Honolatus  Mgaya na katibu  wa  CCM wilaya  ya Ludewa Lusiana  Mbosa walieleza kufurahishwa na jitihada  za  mbunge  huyo katika  kuwatumikia  wananchi wa jimbo  hilo na kuwa utendaji kazi wake unakiwezesha chama  chao kuwa na  nguvu ukilinganisha na majimbo mengine ambayo wapinzani  wameendelea  kujisogeza .

Bw  Mgaya  alisema  mkoa  wa Njombe una  wabunge wengi  ila heshima CCM inavyopata Ludewa   ni kubwa  zaidi na iwapo wabunge  wote  wangefanya kazi kama  mbunge  wa  Ludewa hata  wapinzani  kuweka  bendera  zao katika mkoa  wa Njombe  ingekuwa vigumu .

Huku katibu  wa CCM  wilaya ya  Ludewa Bw Mbosa akiwataka  wananchi  wa Ludewa katika  kuendelea  kukiunga mkono chama  cha mapinduzi ni kupuuza kauli  za  wapinzani ambao wapo  kwa ajili ya  kukwamisha maendeleo  kwa  kupinga kila jema linalofanywa na CCM .

Alisema  kuwa   wapinzani katika  kuonyesha mapungufu yao na  kuwa si  watu  wa kuleta maendeleo ni pale  walipoamua  kususa bunge la katiba huku siku zote  walionyesha  kupigania katiba  mpya  kuwa  kitendo hicho ni kuonyesha kutapenda  nchi  itawalike na  hivyo kuwataka  wananchi  kuwapuuza kwa kutowasikiliza na pindi muda utakapofika basi kuipigia katiba   inayopendekezwa  kura ya ndio .

Kwa upande  wake  mbunge Filikunjombe aliwataka  wananchi hao kuendelea  kumpa ushirikiano zaidi ili  kuweza  kuwatumikia na  kuwa kuongeza  kuwa  lengo lake  kuona posho  anazozipata bungeni kama mbunge zinawanufaisha   wananchi  wake na sivinginevyo .

Alisema kuwa moja  ya  ndoto  yake  katika  kuwatumikia  wana Ludewa imetimia  hivyo kazi  kubwa ya wananchi wa  jimbo hilo ni  kuendelea  kumtumia  zaidi ili kwa  upande  wake kuwasaidia pale  ambapo wananchi hao wanashindwa .

katika ziara   hiyo mbunge Filikunjombe aliweza  kutimiza ahadi yake ya mabati mabati 170, saruji  mifuko  200 ,kitanda cha kujifungulia wajawazito  na darubini  vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya  milioni 15.

No comments: