Tangazo

May 27, 2015

SHEAR ILLUSIONS KUZINDUA VIPODOZI VIPYA VYA LUVTOUCH MANJANO MEI 31 - UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE VIP JIJINI DAR



Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions, Shekha Nasser (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu uzinduzi wa vipodozi vyake vipya aina ya LuvTouch Manjano unatakaofanyika Mei 31 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini. Kushoto ni Ofisa wa Programu wa Manjano Foundation, Gugu Ndlovu na Mshauri Kiongozi wa Manjano Foundation, Sadaka Gandhi.PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

DAR ES SALAAM

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!

Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.
 
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.
 
‘Nina amini kwa kupendeza. Napendelea kulipuka kwenye kila mtoko. Sitegemei vinasaba vyangu. Naamini muonekano mzuri ni kujitolea kwako na kwa wengine pia’ Mwanamitindo toka Somalia, Iman.

Shear Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania kwa Zaidi ya miaka kumi. Tumetanabaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear  Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.
 
LuvTouch Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.
 
SAFARI YA SHEAR ILLUSIONS
 
2005: Duka la kwanza la Shear Illusions ilifunguliwa jengo la Millenium Towers na ilikuwa ni duka la aina yake nchini Tanzania kwa kuuza vipodozi na vifaa vya nywele.
2006: Maduka ya Shear Illusions ilifunguliwa Arusha na Mlimani City
2009: Shear Illusions ilizindua jarida la ‘Shear Hair and Beauty’ inayomlenga mwanamke wa kisasa wa kitanzania.
2013: Duka la Shear Illusions lafunguliwa kwenye jingo la Kibo Commercial Complex, Tegeta
2015: Uzinduzi wa vipodozi aina ya LuvTouch Manjano inayomlenga mwanamke wa kitanzania.
2015: Shear Illusions yazindua taasisi ya ‘Manjano Foundation’ ambayo inajihusisha na kuendeleza program maalum ya kuwawezesha jamii mbali mbali nchi nzima.

Tungependa kushukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI, Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.

Kwa taarifa Zaidi kuhusu tukio hili, tembelea tovuti ya www.manjanofoundation.org na pia kwenye instagram na facebbok.
Kwa kupata tiketi na maelezo mengine unaweza kuwasiliana kupitia barua pepe info@shearillusions-africa.com au info@manjanofoundation.org au simu ya Flora +255 772 999 603.
Asante
Shekha Nasser

KUHUSU SHEAR ILLUSIONS
Shear Illusions ni duka la kitanzania linalouzabidhaa za urembo kwa jumla na rejareja.
Imeajiri wafanyakazi 20 kwenye maduka yaliyopo Milenium Towers (Bidhaa Jumla), Mlimani City Mall na Kibo Commercial Complex, Tegeta. Maduka haya yana bidhaa na vipodozi aina mbali mbali zaidi ya 1000 yanayosambazwa nchini.

1 comment:

Vimax Canada said...

I all the time used to study article in news papers but
now as I am a user of internet so from now I am using net for posts,
thanks to web.