Tangazo

June 24, 2015

Chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania wasitisha kukununua stika za TRA na kupeleka filamu zao Bodi ya filamu kwaajili ya kufanyiwa ukaguzi

 Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa 
Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili.
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu.
 
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

No comments: