Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa
Bayumi (kulia), akimkabidhi seti ya glasi kijana Mariam Mrisho (wa pili kulia)
aliyewezeshwa na Airtel Fursa-Tunakuwezesha vifaa mbalimbali na jokufu kwa
ajili ya kumsaidia katika biashara yake ya mama lishe na kutengeneza vitafunwa
na juisi Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni mama wa Mariam Mrisho, Amina
Lugome. Kushoto ni Ofisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
·Airtel Fursa wiki hii
kuwafaidisha mamia ya vijana Mwanza
AIRTEL
Tanzania kwa kupitia mpango wake kusaidia jamii wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”
imemkabidhi jokofu na vifaa mbalimbali, Mariam Mrisho (23) vyote vyenye thamani
ya milioni 3 ili vimsaidie katika katika biashara yake ya kutengeneza vyakula
‘mama lishe’ na kumuongezea uzalishaji na kipato chake kwa ujumla.
Mariam
Mrisho ni kijana mwingine wa kitanzania kati ya wengi waliofaidika na Airtel
Fursa hivi karibuni kwa kuingia kwenye historia ya kusaidiwa kwa kupatiwa
misaada na wengine kuwezeshwa kwa kuhudhuria warsha za Airtel Fursa kwa lengo
la kuwawezesha vijana hao wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kutimiza ndoto
zao kikamilifu kwa kuwafundisha jinsi ya kupambana na changamoto zinazowakumba.
Akizungumza
baada ya makabidhiano, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi
alisema “Airtel Fursa tunaamini tukiwezesha vijana nchini na wao ni
wataweza kuchangia jamii nzima, vijana wananafasi kubwa sana kwenye jamii.
Hatuishii hapa bali mwishoni mwa wiki tutakuwa Mwanza ‘Rock City’ ambapo pia
tutakutana na mamia ya vijana na tutafanya warsha itayofundisha vijana wetu
mambo mengi ikiwemo jinsi yakupata na kusimamia mtaji, masoko, namna ya
kuendesha biashara au jinsi ya kuzitambua fursa pale waliko”.
“Vijana
wa Mwanza jitokezeni kwa wingi jumamosi hii tarehe 4, tutakuwa pale ukumbi wa
halmashauri ya jiji Mwanza mjini ili tukuwezeshe kwa kugawana ujuzi toka Airtel
Fursa kama tulivyomuwezesha Mariam Mrisho wa Dar” alisisitiza Bayumi.
Kwa
upande wake Mariam ambaye anategemewa na familia yake alieleza kuwa alikuwa
akifanya kazi ya kuajiriwa kwa mama lishe lakini kutokana na kuthubutu na jitihada
zake aliaamua kuacha na kuanzisha biashara yake ya kuuza vitafunwa na ndipo
akasikia habari za Airtel FURSA na akaamua kuainisha changamoto zake na
kuzituma ili kuingia katika mpango huo.
“Nilishajitoa
kufanya shughuli za mama lishe nikiwa nimeajiriwa baada ya hapo nikaamua
kuingia katika shughuli zangu mwenyewe na nikajikita zaidi katika kuuza
vitafunwa, nilijitahidi sana kudamka alfajiri ili kufikia malengo yangu ya mimi
pia kusaidia jamii yangu lakini nikajikuta napambana na changamoto za ukosefu
wa vifaa hivi vyote, kwa kweli iliniwia ngumu kwa kiasi fulani lakini leo
nawashukuru sana Airtel Fursa wameniona baada ya mimi kuandika maombi
yangu kwao”. Alieleza Mariam
Kwa kweli nitafanya kazi kikamilifu ili
niwe balozi bora na baadae niweze kusaidia hata wenzangu wenye mahitaji kama
yangu” alisisitiza Mariam
Bayumi
pia aliwataka vijana toka mikoa yote ya kanda ya ziwa kufika kwa wingi ili
wakutane na wataalam wa Airtel Fursa huku akielekeza kuwa bado Airtel Fursa
inapokea maombi ya vijana wanaotamani kusaidiwa toka mahali popote katika namba
yao ya sms ya 15626 au wanaondika barua pepe kwenda airtelfursa@tz.airtel.com
kwa kuandika jina, umri, mahali anapoishi pamoja na aina ya biashra
wanayofanya ili kuweza kupitiwa na kuwezeshwa na Airtel.
No comments:
Post a Comment