Na Anna Nkinda – Nairobi,
Kenya
Asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia 12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75 na asilimia 90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na umri wa chini ya miaka 40.
Hayo yamesemwa na Rais wa
Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta (pichani), wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa
marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni
mlango wa kizazi, matiti na tezi dume unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Kenyatta (KICC) uliopo mjini Nairobi.
Rais Kenyatta alisema Ripoti
ya saratani iliyotolewa mwaka 2014 na Shirika
la Kimataifa la kutafiti saratani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani
(WHO) ilionyesha takwimu mpya za saratani zinaongezeka kila mwaka na kwa upande wa Afrika vifo vingi vinatokana na saratani ya mlango wa
kizazi.
“Watu wanapoteza maisha
na kuugua saratani kutokana na kutokuwa na uelewa wa ugonjwa huo, kutokuchukua
hatua za mapema na watu kutambulika kuwa
na ugonjwa wa saratani wakati umefikia hatua ya mwisho kutokana na hili
tutaendelea kuwa na wagonjwa ambao wanapata maumivu, wanashindwa kupata
matibabu kwa wakati na uangalizi wa
karibu katika bara letu”.
Ni lazima tuhakikishe
jamii inajulishwa kuhusu ugonjwa wa saratani na
kubadilisha aina ya maisha tunayoishi kama watu wataacha kuvuta sigara,
watakula vyakula vyenye afya, atapunguza kunywa pombe na kufanya mazoezi mara
kwa mara tutakuwa tumezuia asilimia 40 ya saratani”, alisema.
Aidha Mhe. Rais Kenyatta alisema
katika bara la Afrika ugonjwa wa saratani siyo moja ya agenda inayopewa
kipaumbele katika masuala ya afya ukilinganisha na magonjwa mengine kama
ya kuambukiza lakini sasa ili kupambana na saratani kunatakiwa
kuwa na mikakati kwa nchi chache ambazo zitaweza kukutana na kufanya utafiti na kutoa matibabu ili kuzuia
watu wasife na hivyo kuokoa maisha katika hatua ya mwanzo ya ugonjwa.
Mhe. Rais Kenyatta alimalizia kwa kusisitiza kuwa watu wanahitaji kupata chanjo ya hepatitis ambayo inazuia saratani ya Ini na Human Papilloma Virus (HPV) inayozuia saratani ya mlango wa kizazi ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya saratani katika bara la Afrika.
Mhe. Rais Kenyatta alimalizia kwa kusisitiza kuwa watu wanahitaji kupata chanjo ya hepatitis ambayo inazuia saratani ya Ini na Human Papilloma Virus (HPV) inayozuia saratani ya mlango wa kizazi ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya saratani katika bara la Afrika.
Akiwakaribisha wake wa marais na wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria mkutano huo Mke wa Rais wa Kenya Mhe. Mama Margaret Kenyatta alisema ni muhimu wadau hao wakaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na magonjwa hayo ya saratani.
Mhe. Mama Kenyata ambaye
ni Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa
ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume kwa
mwaka 2015 – 16 alisema wamefanikiwa kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa
ya saratani wanachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze
kujichunguza dalili za awali za saratani na kutibiwa kuzuia kwani saratani
nyingi zikigundulika mapema zinatibika.
Alisisitiza, “Tunatakiwa
kuwashawishi viongozi, Serikali na sekta binafsi na taasisi zisizo za
kiserikali kuchukua hatua za lazima ili kuweza kukabiliana na saratani na hivyo
kuokoa maisha ya watu wetu”.
Kuhusu ulaji wa vyakula
alihimiza ni muhimu waafrika wakaangalia maisha ya zamani na kurudi nyuma kwa kuanza kula vyakula vya asili na kuacha kula vyakula vilivyosindikwa hasa kwa vijana”
Mkutano huo wa siku tatu wenye kauli mbiu ya wekeza kuokoa maisha: wajibu wa ushirikiano wa sekta binafsi ulihuhuriwa na wake wa Marais kutoka nchi 12 akiwemo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete.
MwishoMkutano huo wa siku tatu wenye kauli mbiu ya wekeza kuokoa maisha: wajibu wa ushirikiano wa sekta binafsi ulihuhuriwa na wake wa Marais kutoka nchi 12 akiwemo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete.
No comments:
Post a Comment