MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Dansi nchini, Ramadhani Masanja
"Jenerali Banza Stone " (pichani), amefariki Dunia leo nyumbani
kwao Mtaa wa Sinza D, jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa Mujibu wa Mmoja wa wanafamilia ya Marehemu,
Banza anataraji kuzikwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Sinza.
Daily
Mitikasi Blog inatoa pole familia ya Banza na wapenzi wote wa muziki wa dansi nchini.
Mungu aiweke roho yake mahali panapostahili. AMEN
JENERALI BANZA STONE AMETOKA WAPI!!
Ramadhani Masanja 'Jenerali Banza Stone"
Alizaliwa Oktoba 10, 1972 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam
20/10/1972 akiwa ni mtoto wa Mwisho katika familia ya Mzee Ally Masanja
iliyokuwa na watoto nane.
Akiwa anaishi Lumumba, Banza alipata elimu yake ya msingi Shule ya Mnazi mmoja kabla ya kuingia kwenye sanaa ya muziki.
Alikuwa akisoma pia elimu ya dini ambayo aliishika sana na hata akiwa madrasa alikuwa akiimba sana kaswida na akaamua kuanza mziki kwa kushiriki katika vikundi vya mtaani.
Alianza muziki katika kikundi cha disco kilichoitwa Octimas na baadae alihamia kundi cha DBR na mwaka 89 akaanzisha kikundi cha disco cha Home boys akiwa na Elvis Danger (mpwa wake), Ashura Mponda na Ras Dee.
Mwaka 92 akaenda kusoma muziki chuo cha Korea Culture alipomaliza akapiga deiwaka Twiga band kabla ya kuanza rasni muziki na Afri Swez.
Kipaji kilipozidi kupanda akaenda African Stars Twanga Pepeta, TOT, akarudi Twanga na baadae akaanzisha bendi yake ya Bambino Sound hii ikiwa ni mwanzoni mwa 2000.
Banza hakudumu na bendi yake akahamia Chipolopolo, akarudi tena kuifufua Bambino lakini haikusimama akarejea Twanga na kukaa kidogo kabla ya kwenda kuungana na swahiba wake Ali Choki aliyeanzisha Bendi ya Extra Bongo na mpaka anafariki dunia bendi yake ya mwisho kuifanyia kazi ni BM.
Akapata deiwaka na Bendi ya Rungwe iliyokuwa na maonesho yake mjini Mbeya na show ya mwisho ni mwezi Februari mwaka huu alipougua na kurejeshwa kwa ndege jijini Dar akaendelea kuumwa mpaka anafariki leo.
Banza Stone ameacha mtoto mmoja aitwae Haji Ramadhani Masanja.

No comments:
Post a Comment