Tangazo

July 6, 2015

BENKI YA CRDB YARAHISISHA MAISHA VIWANJA VYA SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam. Benki ya CRDB inatoa huduma za kibenki katika maonyesho hayo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti kwa wateja wapya na kutoa huduma za kuweka na kutoa fedha katika tawi linalotembea iliyopo katika viwanja vya Sabasaba. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma (Na Mpiga Picha Wetu) 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki katika tawi linalotembea lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma katika Viwanja vya Sabasaba wakati wa Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mteja akiweka sahihi ya dole gumba baada ya kufungua akaunti ya Benki ya CRDB.
Huduma za kibenki zikiendelea katika Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa.
Mkurugezi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na msanii wa kughani, Mrisho Mpoto wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Mwambapa.  

No comments: