Tangazo

July 8, 2015

JOSHUA NASSARI APATA AJALI YA HELKOPTA JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari (pichani), amenusurika kifo baada ya ndege aina ya helikopita aliyokuwa amepanda kudondoka akiwa katika ziara katika jimbo lake lilipo mkoani Arusha.
 
 Hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo, na Mbunge Nassari pamoja na Rubani wake wako Hospitali ya Seriani mkoani Arusha kwa matibabu baada ya kupata majeraha kwenye ajali hiyo.

No comments: