Tangazo

July 26, 2015

‘Wazazi Nipendeni’ awamu ya pili yazinduliwa Dar

Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Neema Rusibamayila (katikati), wakati alipokuwa ametembelea mabanda ya watoa huduma za afya ya jamii katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni uliofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Ana Bodipo Memba, ambao ni wadhamini wa uzinduzi huo na (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya, Dk.Georgina Msemo. Wengine ni washauri wa masuala ya afya ya jamii.
Mshauri wa masuala ya Malaria kutoka Taasisi ya Jhpiego, Jasmin Chadewa (kushoto), akitoa huduma ya kumpa dawa ya vitamini A, mtoto Rahim Simai,  kwenye uzinduzi wa kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili uliofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ikiwa ni utoaji huduma wa elimu ya afya kwa wajawazito na matumizi ya dawa aina ya SP, upimaji wa malaria pamoja na matumizi ya vyandarua.


Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Ana Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni uliofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulifanyika kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Wengine ni wadau wa sekta ya Afya waliohudhuria uzinduzi huo
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 
Awamu ya pili ya Kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni , Onyesha Upendo’ imezinduliwa Jijini Dar es Salaam huku sasa ikijumuisha pia mwaka mmoja wa kwanza wa maisha ya mtoto.

Hii ni kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya kameni hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Shirika la USAID kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya uzazi wa afya zikiwemo kampuni za simu ambazo zilitoa huduma ya bure ya ujumbe mfupi kutangaza kampeni hiyo.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt, Neema Rusimayila    katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke Jijini Dar es Salaam.
Alisema kampeni hiyo imesaidia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito, watoto wachanga na pia kuhakikisha watoto wanaozaliwa wana afya njema kwa kuhakikisha kina mama na wenza wao wanafuata hatua zote za afya ya uzazi.

“Hapa Tanzania, idadi ya vifo vya watoto ni 51 kwa kila 1000 wanaozaliwa ambayo bado ni kubwa ikilinganishwa na malengo ya serikali kupunguza idadi hii hadi wane kwa kila 1000 wanaozaliwa,” alisema.

Alisema kutokana na idadi hii ya vifo ambayo bado inaisha kidogo, kuna haja ya kuendelea kuweka nguvu katika kampeni hiyo na kutaka mikoa yote na halmashauri zake kuhakikisha wanaipa kampeni hiyo kipaumbele na kuitekeleza ipasavyo ili kuhamasisha kina mama na wenza wao kufuata hatua za afya ya uzazi.

“Tunaamini kuwa awamu hii ya pili itaharakisha patikanaji wa habari kuhusu uzazi wa afya ili kupunguza vifo huku akiongeza kuwa Chuo Kikuu cha John Hopkins pia kimeungana na Shirika la USAID na wizara pamoja na wadau wengine katika kutekeleza awamu hiyo ya pili na kuhakikisha inafanikiwa,” alisema.

Mwakilishi wa Shirika la USAID, Bi. Ana Badipo-Memba alisema wameridhika na mafanikio yaliyopaikana ndani ya miaka miwili ambayo kampeni hiyo imefanyika.

“Leo ni muendelezo wa mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya kampeni hii ambayo ililenga kuwahamasisha kina mama waja wazito na wenza wao kuchukua hatua zinazotakiwa katika kuhakikisha wanazingatia uzazi wa afya na pia kujifungua salama, alisema huku akisisitiza kuwa katika awamu ya pili kampeni hiyo pia itajikita katika muangalia maisha ya mtoto katika mwaka wake wa kwanza.

Kauli mbiu ya awamu hii ya pili ya Kampeni hiyo kwa mujibu wa USAID, ni ‘Onesha Upendo wako.

“Wazazi Nipendeni awamu ya pili itawafikia kupitia njia mbalimbali zikiwemo redio, TV na magazeti. 

Alisema kampuni za simu zitaendelea kutoa huduma ya ujumbe mfupi bure ili kutangaza kampeni hiyo na pia zaidi ya vituo vya afya 3500 vimekubali kubandika matangazo ya kampeni hiyo.

No comments: