Tangazo

September 21, 2015

CHAMA CHA AFYA YA JAMII (TPHA) CHATOA ELIMU DHIDI YA KUPAMBANA NA TUMBAKU KWA VIJANA WADOGO DAR

Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph). 

  Na Andrew Chale, modewjiblog [Dar es Salaam] Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae. 

  Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi.

Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe. 

  Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia. “Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye. Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.

Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.

Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara.

“Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi. Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana. Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige. 

  Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
Mwalimu Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake. 

  Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo.

Mradi huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani. 

  Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini. 

  Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano. Kwa upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.
Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku. DSC_0019
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
Kikundi cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi hatari ya Tumbaku.
Wanafunzi wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
Bernard Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
Shairi mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Mwanafunzi wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango (kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
Wawili kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani ni hatari kwa afya za binadamu
Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
Afisa Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.

No comments: