Afisa Masoko wa Airtel kanda ya ziwa akiongea na mawakali mara baada ya kuendesha semina inayowapatia fulsa Mawakala wa Airtel Money nchini nzima kupata mikopo kupitia simu zao za mkononi. |
Wakala wa Airtel Money katika maeneo
ya Metro Mwanza, Bwn John Hainga akichangia mada wakati wa semina ya
mawakala inayowapatia fulsa ya kupata mikopo isiyo na dhamana
ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa Mawakala.
Kampuni
ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea kuboresha huduma
zake kwa wateja hususani wajasiliamali wanaojihusisha
na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja na utoaji wa
huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala kupata
mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao
za mikononi.
Airtel
imewakutanisha mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu mbalimbali
za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na ukuzaji
vipato katika biashara zao.
"Ukosefu
wa elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio wengi hapa
nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha mapato
kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi wa taifa
.
Kwa
kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya uendeshaji
biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora ya uendeshaji
biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na dhamana kwa
zaidi ya mawakala 20,000 kote nchini Ili kusaidia kukuza biashara
za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia upatilkanaji
wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda ya ziwa wa
Airtel, Bwana Raphael Daudi.
Kwa
upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo bwana John Paschal
alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma hii ya
Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha biashara
zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji. Lakini pia mafunzo haya
yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara zetu kwa
ufanisi zaidi."
Airtel
katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa wateja wake
imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa mawakala,
huduma itakayowawezesha mawakala wa airtel money kote nchini
kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi
500,000/-.
No comments:
Post a Comment