Tangazo

September 25, 2015

Mtoto apotea na house-girl

Picha ya hivi karibuni ya mtoto Loveness C. Jullu
Familia ya Jullu ya Wazo Hill kwa Msabaha jijini Dar es Salaam inaomba msaada kutoka kwa raia wema ili kufanikisha kumpata mtoto wao Loveness Coletha Jullu aliyepotea nyumbani na msichana aliyekuwa akimlea na kusaidia shughuli za nyumbani.

Wawili hao hawajaonekana tangu juzi Jumanne. Taarifa zimefikishwa katika kituo cha polisi na RPC wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni amekiri kupata taarifa za tukio hilo.

Ikiwa una taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwao tafadhali zitoa kupitia namba hizi: 0715797920 na 0786977615.

Asante.

Binti msaidizi wa kazi za nyumbani (house-girl)

Picha ya awali ya mtoto

No comments: