Tangazo

September 23, 2015

VETA KANDA YA DAR YAFANYA MKUTANO NA WAMILIKI PAMOJA NA WAKUU WA VYUO VYA UFUNDI STADI

 Mratibu wa Veta kanda ya Dar es Salaam Bi. Frorence Kapinga akiwakaribisha wakuu wa vyuo vya ufundi vyenye usajili wa awali wa VETA kanda ya Dar es Salaam kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam. Bw.Habibu Bukko akizungumza jambo wakati wa mkutano la wakuu wa vyuo vya ufundi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa kutano huo. 
 Mgeni rasmi Mwalimu Charles Philemon akizungumza na wakuu wa vyuo na wawakirishi wao(hawapo pichani) wakati alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar
Bw. Asanterabi Kanza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya Mashariki akiwasilisha mada kwa wakuu wa vyuo pamoja na wawakilishi wao(hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano huo ili kukumbushana mmbo ya msingi kwenye uendeshaji wa vyuo hivyo vya ufundi.
Mkutano ukiendelea
 
Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano huo
 
 Picha ya Pamoja


Na Mwandishi wetu


Kongamano la wakuu wa vyuo pamoja na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajiri ya  kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo pata usajiri wa awali  ili waweze kupata usajiri wa kudumu vilevile kupewa hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu ili kupata usajiri huo wa kudumu.

Mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam Mwalimu Charles Philemon  akiongea na wamiliki na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata usajili wa kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki ya kupata hisibati inayoonyesha aina ya kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza, kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili  wao waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.

Kwani watu mbalimbali hupimwa kutokana na stadi zao mbalimbali wanazozipata  katika vyuo vyetu na kwenda nazo katika kuzitekeleza  maeneo tofauti , watu hao ambao wamepita  kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi  VETA ndio watu wenye stadi za kazi kwani hutenda kazi kutokana na elimu na utashi  mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao kupitia vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA. anasema  “kutokana na semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia kuna watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi kwa umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za utoaji mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika mamlaka ya VETA”
Pia aliweza kusisitiza fursa ya kujengana kwa kutembeleana baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya kupata ufanisi zaidi  katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani familia inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana ndani ya VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda mwingi  huwa tunakutana mara moja katika maonesho mbalimbali lakini familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo mbalimbali.

Naye mkurugenzi wa VETA  kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa pamoja na kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza kusema baada ya kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila chuo kiwe kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo ya ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI ni kutambua zile fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo kwenye fani zipi.

No comments: