Tangazo

September 22, 2015

Wananchi wa Kisarawe washiriki mdahalo wa Ajenda ya Watoto kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015


Ndg Abel Mudo, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo ulihusisha pia wakazi wa kata ya kisarawe
Baadhi ya wakazi ya kata wa kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wa  ajenda ya watoto ullohusisha wagombea wa udiwani kupiitia vyama vya ccm na chadema 

Mmoja wa wananchi wa kata ya kisarawe akichangia katika mdahalo wa ajenda ya  watoto kuelekea uchaguzi mkuu  ambapo ulihusisha wanafunzi na wagombea  wa udiwani wa kata hiyo 




         Mwanafunzi Amina Joka akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wanafunzi wa shule za Msingi  chanzige A ,chanzige B na kisarawe  na wagombea wa udiwani kupitia vyama vya ccm na chadema walishiriki

Ndg Abel Mudo ambaye ni mgombea wa Udiwani kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wanafunzi wa CHANZIGE ,na kisarawe 

Mmoja wa wanafunzi wa shule msingi CHANZIGE A akifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto uliowahusisha wagombea wa udiwani wa vyama vya chadema na CCM 

Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi



Picha za Wanafunzi ni za wanafunzi wa shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila zilizopo Kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo huo.


Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi
Ajenda ya watoto ilianzishwa na mashirika ya watoto Tanzania yakiongozwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa nia ya kuhakikisha maswala ya watoto na haki zao yanawakilishwa vyema katika serikali ya Tanzania.


Katika kuhakikisha kwamba Ajenda za watoto zinazungumzwa katika jamii Kipindi cha redio cha Walinde Watoto leo kimeandaa mdahalo uliowahusisha wagombea wa udiwani kata ya Kisarawe ambao ni Abel Mudo (CCM) na Baraka Musa (CHADEMA) na wakazi wa Kata ya Kisarawe ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na mipango ya vyama vyao katika kutatua changamoto hizo.

Mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ulihudhuriwa na wenyekiti wa vijiji, na vitongoji, walimu, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wananchi wakazi wa Kata ya Kisarawe.

Akiinadi Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa anayegombea udiwani kata ya Kisarawe, alisema chama chake kinaamini kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na akasema endapo kitaingia madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba inayotambua na kutaja moja kwa moja haki za watoto.

Naye mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Abel Mudo alisema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha zina walimu wa kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira rafiki na kutoa zana kwa watoto wenye ulemavu.

Mgombea huyo aliahidi kwamba watafanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo  ya mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi kidato cha nne.

Mwanafunzi Amina Joka aliwataka wagombea udiwani hao pindi mmoja wapo atakapochaguliwa, wahakikishe wanajenga hosteli za wanafunzi kufikia kwani kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali mrefu sana kwenda shule hali ambayo ni hatarishi kwani wanakutana na vishawishi vingi njiani. 

Katika hatua nyingine, wagombea hao walipata fursa ya kusikiliza kero za wanafunzi kutoka shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila wilayani kisarawe ambao walitaja kero za upungufu wa walimu, ukosefu wa huduma za afya, adhabu za mashuleni na ukosefu wa maji kama kero zao za mda mrefu. “Mgombea bora ni Yule atakayetuletea maji kwani tunaenda kutafuta maji umbali mrefu badala ya kujisomea” Alisema mwanafunzi mmoja.


Unaweza kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org

No comments: