Tangazo

October 19, 2015

ACACIA YADHAMINI PAMBANO LA SOKA LA VIONGOZI WA DINI NA MABALOZI KUHAMASISHA AMANI

 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo

NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na kutwaa kombe.
Akitoa nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.
Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia  a ustawi wa kampuni,  Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani safi wapenzi wa soka.

 
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili kushoto)


 Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo
 Chikawe, akisalimiana na Alex Lugendo
 "Ball Boys" wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani
 Sheikh Alhadi akiwa kwenye mazoezi ya viungo na viongozi wenzake wa dini kabla ya mpambano huo

 Sheikh Alhadi akifumua shuti


 Mwamuzi wa pambano hilo Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akipuliza kipyenga
 Sheikh Alhadi akijaribu kufunga penalty ambayo hata hivyo hakufanuikiwa kufunga

 Timu ya viongozi wa dini iliyomenyana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
 Timu ya soka ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha mashiorika na nchi zao hapa nchini
 Waziri Chikawe, viongozi wa Acacia, na wale wa TFF wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
 Viongozi wa dini wakiongozwa na kocha wao wakati "wakipasha" kabla ya pambano hilo
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, akiwaeleza waandishi wa habari sababu za kampuni hiyo mudhamini pambano hilo la soka.“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
 "Benchi la ufundi" la viongozi wa dini, kutoka kushoto, Sheikh Basaleh, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, na Sheikh Othman, wakifuatilia kwa karibu pambano hilo
 Nasaha za mgeni rasmi kwa timu zote mbili
 Waziri Chikawe, (kulia), akiongozana na Assa Mwaipopo, (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo, mara baada ya ukaguzi wa timu

 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, (kushoto), ambaye alikuwa kamisaa wa mchezo aisalimiana na Assa Mwaipopo
Mazoezi ya viungo yakiendelea

No comments: