Tangazo

October 8, 2015

CONNECTMOJA TECHNOLOGIES LIMITED WAZINDUA MFUMO MPYA WA SCHOOL MANAGEMENT SYSTEM

Kampuni ya Connectmoja Technologies  inayoendesha shughuli zake hapa nchini Tanzania leo imezindua Mfumo madhubuti unaojulikana kwa jina la  KSchool  Management system.


Akizungumza na wana habari, Mtaalamu wa utafiti na ukuzaji wa Masoko Bw. Fred Crich amewaambia wanahabari kwamba Kampuni yao ya ConnectMoja Technologies  imejikita zaidi katika kuhakikisha inasaidia sekta ya elimu na uwekezaji kukua pamoja na maendeleo ya Teknolojia hapa Nchini.





Bw. Crich amesema mfumo  huu umewalenga wamiliki wa mashule kwani mfumo unawawezesha kuweka rekodi sahihi za wanafunzi, kutunza kumbukumbu za mienendo ya wanafunzi, kuweka rekodi ya matokeo ya wanafunzi na wazazi pia wanaweza kuona rekodi hizi wakiwa majumbani au mahala popote kwa kutumia simu za kiganjani au computer zenye internet; Mfano. Mwanafunzi  anapotoka shule, Mzazi atakuwa na uwezo wa kuingia kwenye  mfumo huu kupitia(Parent Portal) na kujua kama mtoto alifika shuleni, na kama alifika alifundishwa nini, pia kujua kama ana Homework ya kufanya pindi afikapo nyumbani, pia itamwonesha matokeo yake papo hapo.

Mfumo huu una Teachers Portal na students portal ambapo Mwalimu anaweza kutuma Assignments kwa wanafunzi hata wakiwa Likizo.

Bw. Crich ameelezea kwamba mfumo huu umeanza kutumika kwenye baadhi ya shule hapa Nchini na kwa sasa wameuboresha zaidi ili uweze kuwanufaisha wazazi pamoja na wadau wa sekta ya elimu.

Pia anakaribisha wamiliki wa shule wote  wanaotaka kuupata mfumo huu, bei ni nafuu .

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
call: +255 777 88 0000 7  au  0714 215 600

No comments: