Tangazo

October 16, 2015

DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA HELKOPTA


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa na Mgombea pekee wa jimbo hilo katika uchaguzi unaotaraji kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Deo Haule Filikunjombe (43) PICHANI amefariki dunia kwa ajali ya Helkopta.

Mbali na Filikunjombe pia watu wengine wa tatu wamaefariki katika ajali ya chopa iliyotokea jana jioni katika hifadhi ya Selous Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. 

Rubani wa Chopa 5Y-DKK ambaye ni baba wa aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ukongam Jerry Silaa, Capt. William Slaa nae amefariki.

Jerry Silaa amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake ambapo pia Kamanda wa Operation wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuthibisha vifo hivyo vya watu wanne.



Filikunjombe pamoja na wenzake hao walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Ludewa. 
  
Deo Filikunjombe anakuwa ni mgombea wa 6 kufariki tangu akuanza kwa Kampeni za Uchaguzi mwaka 2015 ambapo uchaguzi wake unataraji kufanyika Oktoba 25 mwaka .  

Wagombea hao ni Mohamed Mtoi wa CHADEMA jimbo la Lushoto,  Celine Kombani wa CCM jimbo la Ulanga Mashariki, Estomih Malla wa Chama cha ACT-Wazalendo Mgombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini, Dk Abdallah Kigoda wa CCM Jimbo la Handeni Mjini na, Dk Emmanuel Makaidi wa NLD jimbo la Masasi aliyefariki jana Oktoba 15, 2015.



No comments: