Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Bi. Dangio Kaniki (kulia) akitoa mada kwa Vijana washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa. |
Wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa
walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel
fursa wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Uhusiano na Matukio
wa Airtel, Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel wa mkoa huo.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Baada ya kukata tamaa ya
maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na
kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha
na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSA
Wakizungumza na mara
baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa
Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao
walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa
wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .
Washiriki wa mafunzo
hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema
kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo
hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya
kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .
Alisema Bi Sanga kuwa
sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika
biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya
uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia
mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.
"Wapo baadhi ya
mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili
kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila
kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa
wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee"
Huku Bw Kasim mbali ya
kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema
kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata
mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni
miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.
Kwa upande wake afisa
mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa
Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na
wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24
Alisema kuwa mradi huo
umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa
wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .
Bi Kaniki alitaja mikoa
ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza,
Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi
ya vijana 1700 wamefikiwa.
Alisema kuna njia mbili
za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia
ya pili kupatiwa vitendea Kazi .
Hivyo aliwataka vijana
wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao
basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.
Alisema ili kijana aweze
kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa
kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina,
Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia
barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya
biashara.
Maelezo kuhusu program
ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtelwww.airteltanzania.com
Alisema kuwa Airtel
Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale ambao hawana
shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa kwao .
Aidha alisema kuwa
tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo ambao umelenga kuwainua
vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka huu utakuwa ni mradi endelevu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Iringa
youths empowered by Airtel FURSA
After losing hope in life
for a long time youth in Iringa have expressed appreciation to the Airtel for
providing youth empowerment entrepreneur training on how to establish and run
their businesses profitably through Airtel FURSA program.
Speaking immediately
after the one-day workshop of Airtel FURSA which took place at the Highland
hall in Iringa which involved more than 200 youth, the participants said that
the workshop is a great rescuer for them as this is not the time to stay idle
when there are such opportunities, we must engage in different activities that
will make us benefit from this program. We thanked Airtel today for showing us
another way of changing our lives.
Participants of the
training Ms. Husna Sanga and Mr Okelo Kasim talking on behalf of their
colleagues said that apart from Airtel to provide training to them, not
only helps them acquire knowledge to run a business and other projects but part
of redemption their families around them.
Ms. Sanga said that
most of the young people especially girls were hoodwinked into getting into
relationships with men and engage in business discomforting as the sale of their
bodies due to lack of knowledge of the establishment of small businesses which
will redeem them economically. So through the initiative of Airtel FURSA now
they can change their lives.
"There are some
other girls who are forced to do business of selling their bodies to earn, by
the end of the day they are killed by AIDS, but for us who have received this
knowledge through Airtel FURSA we can be an example to others who think the job
is to sell their bodies particular”
And Kasim, thanked Airtel
for caring for youth in the country and be part of this great initiative. He
promised to be an example to others by working hard and run their businesses
more efficient.
On her part Airtel
Tanzania public relations and events officer Dangio Kaniki commented that through
Airtel FURSA more youth between the age of
18-24years old, will benefit. The initiative is a lifetime opportunity to
sustainably nurture business ideas, serve communities and reduce unemployment
in the country.”
She said that the project
aims at providing opportunities for youth who own and run businesses with
relevant business skills and support for sustainable growth.
Ms. Kaniki cited regions
which have already reached with Airtel FURSA program so far
are Mbeya, Arusha , Dodoma , Mtwara , Mwanza , Mtwara, Dar es
Salaam, Morogoro , Tanga, Tabora, and Iringa that so far and more
than 1700 young people have been touched.
She said there are two
ways to enable youth, first by providing entrepreneurship education training
and second by providing tools to bust their businesses.
So she called all the
young people in the country hereby urge the youth to take advantage of this
opportunity and make the most of it as it is provided for free.
She said that in order
for the youth to benefit from or participate in Airtel FURSA will be required
to send SMS to 15626 with the following details: - name, age, type of business
and location. Alternatively interested youth can submit their applications
through FURSA email airtelfursa@tz.airtel.com
Airtel details about the program is available on the
Airtel website www.airteltanzania.com
“This programme targets
young, energetic and enthusiastic business start-ups that are ready to take up
the challenge and grow their businesses. As Airtel we aim at
empowering people’s lives”, added Kaniki.
In addition she said that
already some of youth around the country have received grants from the program
which aims to lift up their lives, adding that the project was started this
year in May and will be an ongoing project.
No comments:
Post a Comment