Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay
Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki
kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod,
wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili
eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na
wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia
kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco,
wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya
usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa
Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki
kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya
usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa
Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali
waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha zoezi la
usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka
eneo la Morocco, baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa eneo hilo la
kufanya usafi wa mazingira leo.
**************************************
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anwani ya simu:
“MAKAMU”, Barabara ya Luthuli,
Simu Na. +255
2116919
P.O Box 5380,
Fax Na. +255
2116990 Dar es Salaam.
Barua Pepe: km@vpo.go.tz TANZANIA.
09/12/2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo
ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na
Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 ya uhuru wa
Tanzania Bara.
Akizungumza
na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais
amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni
wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.
“Haya
makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha
hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema Mhe. Samia.
Alielezea
kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo
alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za
mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.
Makamu
wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni
michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na
kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa
na elimu bora.
Pamoja
na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa
Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya
DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar
es salaam
No comments:
Post a Comment