Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, (wapili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015. Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh. Angela Kairuki.
Na
K-vis Media/Khalfan Said
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali
katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za umma.
Msaada
huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoa
kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu
waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini
hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa viotanda, alisema
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa
ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na
kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya
matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.
Kufuatia
maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Akipokea
vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke,
Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF,
kwa moyo huo wa kusaidia jamii.
“PSPF
mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri
kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.”
Alisema
Mbunge wa viti Maalum, Angella Kairuki, (wapili kulia),
akipokea msaada wa vitanda, kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul
Njaidi, kwenye hosptali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Desemba 7,
2015. Mfuko huo umetoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka ili kuunga mkono
juhudi za serikali za kumaliza tatizo la vifaa tiba kwenye hosipatli za umma.
Kulia ni .. Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo
Njaidi (kulia), akiangalia wakati fundi akiunganisha moja ya vitanda hivyo wakati wa makabidhiano hayo
Njaidi akisaidiana na Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo, kuweka sawa shuka kwenye kitanda
Mh. Angela Kairuki, (wapili kulia), akimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kukabidhi vifaa hivyo. Wengine kushoto ni maafsia wa PSPF
Mh. Kairuki akipatiwa maelezo juu ya huduma zilizochapishwa kwenye kipeperushi cha PSPF
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mganga mkuu wa wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, akitoa nasaha zake
Mh. Kairuki (kulia), akijadiliana jambo na mafisa wa hospitali ya Temeke na uongozi wa wilaya pamoja na Afisa Uhusiano wa PSPF, Bw. Njaidi
Wafanyakazi wa hospitali hyo wakibeba sehemu ya vitanda hivyo
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema, akipena mikono na Bw. Njaidi wakati akimshukuru kwa msaada huo
Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment