Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,
TPB, Sabasaba Moshingi, (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi kwa Mkurugenzi wa
Shirika la Vijana Wajasiriamali na Uwezeshaji Tanzania, (TYEEO), Ayub Gerald
Luhuga, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Wizara ya Fedha na Mipango, jijini
Dar es Salaam Desemba 23, 2015. Benki hiyo imevipatia vikundi vinane vya
wajasiriamali jumla ya shilingi milioni 244,500,000/- kama mpoko nafuu ikiwa ni
awamu ya kwanza ya utoaji mikopo hiyo, kufuatia makubaliano baina ya benki hiyo
na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), kudhamini vikundi
hivyo ili vifungue akaunti TPB na kujipatia mikopo huku NEEC ikiwa ndio
wadhamini wakuu. Jumla ya shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa lengo hilo.
Wanoshuhudia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa NEEC, Anna Dominic, (wapili kushoto)
na afisa wa baraza hilo
Bw. Moshingi akisalimiana na wana VICOBA
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
BENKI
ya Posta Tanzania, TPB, imekabidhimkopo wa jumla ya shilingi milioni 244,500,000/- kwa
vikundi vinane vya wajasiriamali.
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo Desemba 23, 2015 kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam, ambapo
mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, (NEEC).
Akizungumza
kwenye makabidhiano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi
alisema, fedha hizo ni awamu ya kwanza ya benki kutoa mikopo hiyo yenye
masharti nafuu, baada ya kutiliana saini na NEEC Julai mwaka huu wa 2015,
ambapo baraza hilo litadhamini vikundi hivyo ambavyo vitapaswa kwanza kufungua
akaunti TPB kabla ya kupatiwa mikopo hiyo ambayo jumla ya shilingi bilioni 2
zimetengwa kwa dhumuni hilo.
“Ninayo
furaha kubwa kuwakabidhi nyinyi wajasiriamali ili muweze kutimiza ndoto zenu za
kujikwamua kiuchumi.” Alisema Bw. Moshingi na kuhimiza vikundi zaidi vya wajasiriamali kujiunga na benki hiyo ili navyo
vifaidi kwa wanachama wake kujiongezea mitaji kwa ajili ya shughuli zao za
kiuchumi.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi.
Anna Dominic, alisema, baada ya NEEC kuona takwimu zinaonyesha kuwa hapa nchini
ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto kubwa kabisa na hivyo inahimiza wananchi
kujiunga kwenye vikundi ili NEEC kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama TPB,
kuweza kuwapatia mikopo kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi.
“Ningependa
kuwaasa wajasiriamali mliopokea mikopo hiyo, kufanya kazi kwa bidii kama ulivyo
msimamo wa serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
ya “Hapa Kazi Tu”.” Alisema na kuwahimiza kutumia vizuri mikopo hiyo kwa
shughuli zilizokusudiwa ili waweze kurejesha tena kwa wakati.
Akitoa
shukrani zake baada ya kupokea mkopo huo kwa niaba ya wenzake, Mkurugenzi wa
Shirika la Vijana Wajasiriamali na Uwezeshaji Tanzania, (TYEEO), Bw. Ayub
Gerald Luhuga, aliishukuru TPB kwa kuwaunga mkono katika kuhakikisha
wajasiriamali wanakuza mitaji yao ili kujikwamua kiuchumi, na kuahidi kuwa
mikopo hiyo itatumika kama ilivyokusudiwa na kurejeshwa kwa wakati.
Bi. Anna akitoa hotuba yake
Mkurugenzi wa Idara ya
Mikopo ya TPB, Bw.Henry Bwogi, (kulia), Mkurugenzi wa Masoko wa TPB,
Bw.Deogratius Kwiyukwa, (katikati), na Meneja Mikopo ya Vikundi ya TPB,
Bw.Ramadhan Liganga, wakibadilishana mawazo
Bw.Moshingi, (kushoto), akimsikiliza Bw. Kwiyukwa, huku Afisa Habari Mwandamizi wa TPB, Bw.Theo Mwakifulefula akisikilzia
Mmoja wa wajasiriamali akipiga makofi kufurahia jambo
Mkurugenzi wa Idara ya
Mikopo ya TPB, Bw.Henry Bwogi,(kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa TPB,
Bw.Deogratius Kwiyukwa, (katikati), wakimsikiliza mkurugenzi wa TYEEO, Bw. Ayubu
Bw. Ayubu akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajasiriamali wenzake
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment