Mkuu wa wilaya ya Babai Mkoani Manyara,
Crispin Meela akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki kwenye
mafunzo ya biashara yaliyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Fursa
wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
MANYARA
Mkuu wa wilaya ya Babati
Mkoani Manyara, Crispin Meela amewataka vijana mkoani humo kuchangamkia fursa
ya mafunzo ya ujasiriamali na msaada wa vifaa vya kuendeshea biashara
vinavyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, kupitia mradi wake wa
Airtel Fursa.
Meela ametoa wito huo mjini Babati mkoani MANYARA, wakati
akifungua mafunzo ya siku moja ya Aritel Fursa ambapo zaidi ya vijana 200
wameshiriki mafunzo hayo.
Amewahimiza vijana hao kubuni miradi inayohusiana na kilimo kwa
kuwa sekta hiyo ndio yenye uhakika wa kuajiri idadi kubwa ya watu hivyo
kujikwamua kiuchumi.
"Ni lazima vijana muwe wabunifu na mjiunge kwenye vikundi vya
wajasiriamali ili muweze kutumia vizuri fursa zinazotolewa na Airtel pamoja na
serikali kufanyabiashara kwa viwango vinavyokubalika" amesisitiza Meela.
Aidha ameongeza kwa kusema mafunzo haya ambayo yanatolewa bure kwa
vijana yatachangia kiasi kikubwa katika kupata ujuzi na kuboresha uendeshaji wa
biashara zao na kuongeza ufanisi. Na kuwapongeza sana Airtel kwa kuwekeza
katika vijana mbalimbali nchini.
Akizungumza na vijana hao, Meneja huduma kwa jamii Bi Hawa Bayumi
amesema kuwa vijana wengi zaidi wanatarajiwa kufikiwa nchini kote katika awamu
ya pili ya mradi huo.
Amesema Airtel Fursa haitoi mikopo bali vijana watakaokidhi vigezo
watapatiwa ruzuku itakayotumika kununua zana zitakazotumika kuinua uzalishaji
katika miradi wanayoiendesha.
"Kuna timu ya wataalamu watakaopitia
miradi itakayowasilishwa ambao watapitia vigezo vilivyoainishwa na washindi
watasaidiwa vifaa ili ndoto zao za kujikwamua kiuchumi ziweze kutimia'
Alisisitiiza Bayumi.
"Katika awamu ya kwanza ya Airtel
Fursa tuliweza kuwafikia vijana 2500 kupitia mafunzo kama haya tunayoya fanya
Leona vijana 13 walifanikiwa wakawezeshwa kwa kupewa vitendea kazi na hivi sasa
wanafanya vizuri katika biashara zao".
Amesema AIRTEL imefanya utafiti nchi nzima
na kubaini changamoto lukuki zinazowakabili vijana ikiwemo ukosefu wa mitaji,
ubunifu na elimu ya Ujasiriamali ndio maana ikaamua kuwekeza katika kundi hilo.
"Tunaamini kuwa vijana watakao
saidiwa watakuwa chachu ya kuwawezesha vijana wengine kwa kuwaajiri na baada ya
miaka michache vijana watakuwa wamejikwamua kiuchumi na kuondokana na
umasikini" aliongeza Bayumi.
Amewashauri vijana nchini kote
kuchangamkia fursa hiyo kwa kujipatia elimu ya ujasiriamali inayotolewa na
kampuni yake ili waweze kufaidina mradi huu.
No comments:
Post a Comment