Tangazo

January 15, 2016

Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar

Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.

· Ni duka lenye muundo na mazingira ya kisasa
Dar es Salaam 

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka la kisasa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora tofauti na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake

Duka hilo la kisasa liko katika ofisi za makao makuu ya Airtel barabara ya Moroco

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema” Tunayodhamira ya kuwa karibu na wateja wetu ili kuwapatia huduma bora zinazokidhi mahitaji yao.  duka letu jipya tulilolizindua leo litakuwa na sehemu maalumu itakayowawezesha wateja wetu kuona bidhaa bora za mawasiliano zikiwemo simu za aina tofuati na kupata nafasi ya kuzijaribu kwanza ili kuona ubora wake na kufanya chaguo la ununuzi. tunaamini wateja wetu sasa wateweza kufurahia huduma zetu kwa kuwa watapata nafasi ya kuchagua aina ya kifaa au simu wanayomudu kuitumia kwa urahisi zaidi”.

“Duka letu la Airtel Expo litakuwa ni sehemu ya maonyesho na ubunifu kwa wateja wale wanaopenda kuishi maisha yanayoendana na technolojia ya kisasa ndani ya sekta ya mawasiliano. Kila atakaetembelea duka hili atafurahia huduma za haraka toka kwa watoa huduma wetu ambao watatatua mahitaji na matatizo yao katika mazingira ya kirafiki zaidi” alieleza Colaso

Akizindua duka hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani alisema “Ninawapongeza sana Airtel kwa kutengeneza duka hili la kisasa na kibunifu litalorahisisha utoaji huduma kwa wateja na watumiaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea matumizi ya  technologia ya mawasiliano katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi ”

“Natoa wito kwa wakazi wa Dar es saalam na wateja wa Airtel kutembelea duka hili na kufurahia mazingira bora na kuunganishwa na huduma za kifedha na huduma zote za mawasiliano nilizoziona hapa. alimaliza kwa kusema Mh, Ngonyani

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja , Adriana Lyamba alisema “Duka letu litakuwa linatoa huduma kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa muda saa 3 hadi saa 11 jioni na Jumamosi kuanzia saa 3 hadi saa 7 mchana. Huduma zote muhimu kama Airtel Money, huduma ya intanet, bidhaa za kisasa kwa Intaneti na  vifaa vya Wi-Fi yaani (Home Wi-Fi)  pamoja simu za smartphone za vitapatikana katika duka letu.”

Adriana aliongeza kwa kusema Duka letu la Airtel Expo lina sehemu maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wateja watu maalum yaani (Airtel Premeir Custumers) ambapo mteja anaweza kupitia na kusaini mikataba wake au kulipia ankra yake, kurudisha namba iliyopotea, huduma za Airtel Money na nyingine nyingi zitatolewa.”

Kuzindulia kwa duka hili ni muendelezo wa kutimiza dhamira na mkakati wa Airtel wa sasa wa kukamilisha maduka 28 yanayoendelea kutengenezwa na kuzinduliwa nchi nzima hadi ifikapo  Juni mwaka huu.

No comments: