The
founder and Chairman of Apollo Hospitals Dr. Prathap .C. Reddy.
Mara nyingi watu kutoka nchi zilizoendelea
waishio na tatizo la damu na upungufu wa kinga mwilini huishi, tofauti na nchi
zinazoendelea ambazo zinakumbana na uhaba wa huduma ya kupandikiza uboho.
Huduma za kisasa na bora za kupandikiza
uboho katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ni tatizo; kusubiria huduma
bora katika nchi hizi zinazoendelea, inaendelea kuhusiana na hali mbaya ya
kiafya na vifo. Hii ni kutokana na ripoti mpya za kiafya. Kutokana na takwimu
za mwaka 2012, ni nchi tatu tu za kiafrika ambazo ni Misri, Afrika kusini na
Nigeria ambazo zina hospitali zenye uwezo wa kupandikiza uboho.
Upandikizi wa uboho ni njia mpya ya
kisayansi na udaktari katika kutibu matatizo na maradhi kama Leukimia, kuvimba
kwa seli (Lymphoma), saratani katika seli nyeupe (Multiple myeloma), sicko seli
anaemia, kuharibika kwa uboho (Aplastic anaemia), Thalassemia, ukosefu wa seli
nyeupe (Congenital neutropenia), na upungufu wa kinga za mwili. Matatizo maalum
kama ya uvimbe na ulemavu wa kurithi kama Thalassemia pia umepatiwa ufumbuzi
mzuri kupitia matibabu haya.
Upandikizwaji wa uboho na seli za mfumo wa
kati wa damu ni mfumo unaorudisha seli katika shina la mfupa zilizoharibiwa kwa
matumizi makubwa ya mionzi ya kuulia saratani na mionzi mingine pia. Baada ya
kupatiwa tiba kwa dozi yenye nguvu ya dawa za saratani na mionzi, mgonjwa huwa
anatengeneza shina bora la seli, zinazo safiri kwenye uboho na kuanza
kutengeneza seli mpya za damu.
Kwa mujibu wa daktari mtaalamu wa upasuaji
Tanzania Dk. Harrison Chuwa, upandikizwaji wa uboho ni wa muhimu sana
kulinganisha na madhara ya kutokufanya hivyo kama kupata magonjwa ya leukaemia,
seli kuvimbiana hasa kwa kesi za kupooza kwa viungo vya mwili.
“Upandikizwaji wa uboho ndio tiba ya
mwisho kwa wagonjwa wenye saratani ya damu,watanzania wengi huwa wanapewa rufaa
ya kwenda kufanya upandikizwaji katika hospitali za Apollo India kwa
kudhaminiwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii” Alisema
Dk. Chuwa.
Ufanano katika uboho au seli za damu
unaokusanywa kutoka kwa wanaojitolea damu kwa wagonjwa wanaohitaji inaweza
kuokoa maisha ya wagonjwa zaidi ya asilimia 70.
Wastani wa gharama za kufanya upandikizaji
wa uboho kwa nchi zilizoendelea ni kati ya dola za kimarekani 50,000 mpaka dola
1,000,000 kulingana na aina ya hospitali unayofanyia. Kwa nchi kama Singapore,
Malaysia, Brazil, Mexico, India, Thailand, Hong Kong gharama ni kati ya dola za
kimarekani 20,000 mpaka 60,000 kulingana na aina za hospitali.
Kwa mujibu wa www.patient-help.com, Marekani na Ulaya wanatoa huduma ya gharama zaidi ya upandikizwaji wa
uboho kwa dola 200,000 na upandikizwaji kwa kupata mtoaji damu anayefanana na
kundi lako ni dola 250,000. Hii ni tofauti na India ambao wanatoa huduma hiyo
ya kwanza kwa dola 35,000 na ya pili kwa dola 50,000.
Mbali na kupewa cheti kutoka JCI hospitali
za Apollo nchini India zinatoa matibabu bora kabisa kwa kutumia vifaa vya
kisasa na kwa bei nafuu kulinganisha na mataifa ya Ulaya na Marekani. Kutokana
na uhitaji wa upandikizwaji wa uboho duniani kote, hospitali za Apollo
zimezindua huduma maalum ya upandikizwaji wa uboho. Kitendo hicho kimeifanya
hospitali hii kuwa kitengo cha kiteknolojia katika afya bora.
“Hospitali za Apollo zilifungua
milango yake mwaka 1983 na kutambulisha huduma bora za kimataifa nchini India,
kwa gharama zilizo chini sana kulinganisha na zile za ulaya. Hii ni mara ya
kwanza kwa hospitali za Apollo kuchukua jukumu kubwa hilo la kiafya na
kuifanya kuwa hospitali kubwa ya kwanza kutumia teknolijia ya hali ya juu
katika matibabu”. Aliyasema hayo mwanzilishi na mwenyekiti wa hospitali za
Apollo Dk. Prathap.C. Reddy.
Kituo cha upandikizwaji wa uboho katika hospitali
za Apollo, kimefanikiwa kufanya zaidi upandikizaji 700 kwa mafanikio ya
hali ya juu. India ni nchi inayosifika kwa upandikizwaji kwa wagonjwa wanaotoka
mataifa mbalimbali, kwa sababu sio tu kwa kwamba hospitali hizi zina timu za
madaktari bingwa wa upandikizaji bali pia wana njia nyingi bora za kuzuia
madhara ya kiafya katika zoezi hilo.
Tanzania ni kati ya nchi iliyonufaika na
vituo vya afya kutoka hospitali za Apollo. Katika mahojiano siku za
karibuni na mgonjwa aliyetambulika kwa majina ya Dk. Philip Robert Hiza ambaye
baada ya kugundulika ana tatizo la seli alipewa rufaa kwenda hospitali za
Apollo ambapo alipatiwa matibabu kwa miezi mitano yanayohusisha
upandikizwaji wa uboho pia, Dk. Philip Robert Hiza alikiri kuwa upandikizwaji
wa uboho umeleta mafanikio makubwa katika maisha yake.
Maendeleo haya katika matibabu yamepunguza
kiwango ha muda uliokuwa unatumika hospitalini kwa ajili ya mgonjwa kupata
nafuu. Na kupata nafuu ndani ya muda mfupi kunapunguza gharama za matibabu pia.
No comments:
Post a Comment