Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Ndugu Asumsyo Achacha akizungumza ofisni kwekwe juu ya zoezi linaloendelea la kuwasaka wahamiaji haramu mkoani humo.
|
Na Jamiimoja blogu, Mbeya
Zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi
bila kibali limeendelea kufanikiwa mkoani Mbeya ambapo jumla ya wageni 20
wamekamatwa mkoani humo kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la kuingia
nchini kinyume cha sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwakwe Afisa uhamiaji Mkoa wa mbeya Ndugu
Asumsyo Achacha amesema hatua hiyo imefanyika ikiwa ni kutekeleza majukumu yao
ya kila siku sanjali na kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt
Charles Kitwanga alilotoa hivi karibuni.
Aidha
amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya ya kuratibu ajira za wageni ,Sherii Na.1 ya
mwaka 2015 ambayo inawataka wageni wote walioajiliwa hapa nchini kuwa na vibali
vya kazi na hati za ukaazi nchini.
Afisa
uhamiaji huyo amewataja raia hao waliokamatwa katika msako huo ni pamoja wakenya
watatu (3)wamalawi 14 pamoja na wakongo watatu (3).
Aidha
amesema kuwa mwaka 2015 jumla ya wahamiaji haramu 478 kutoka mataifa mbalimbali
walikamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali
ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini.
Amesema
mbali na changamoto zilizojitokeza ikiwemo upungufu wa vitendea kazi ,fedha
pamoja na rasilimali bado shughuli za
uhamiaji mkoani humo ziliendelea kufanyika kama kawaida na kwa ufanisi mkubwa.
Pia Afisa
Uhamiaji huyo amebainisha kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ofisi yake
itahakikisha kila mtu aliyevunja sheria anakamatwa hivyo ametoa wito kwa
waajiri kuacha tabia ya kuwapa ajira wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya
kazi na ukaazi kwani msako huo utaendelea katika viwanda ,migodi mashuleni na
mahotelini.
No comments:
Post a Comment