Tangazo

April 11, 2016

Airtel yaleta 'Jipimie Yatosha Yako' kutoa uhuru zaidi vifurushi vya Yatosha

Meneja Msoko wa Airtel, Anethy Muga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha yako” kitakachowawezesha wateja kutengeneza na kununua kifurushi cha wanachokitaka  kutokana na chagua na mahitaji yao. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo  Nahreel akifatiwa na  Aika. PICHA: MPIGAPICHA WETU
XXXXXXXXXXXXXXXX

·   Kwa mara ya kwanza Tanzania unajipimia vifurushi vya Airtel Yatosha UTAKAVYO
·   Jiunge na Airtel ufurahie uhuru wa kujitengenezea kifurushi chako mwenyewe  kwa gharama nafuu

Dar es Salaam 

Airtel Tanzania ili kutoa uhuru zaidi kwa wateja wake imetangaza kifurushi kipya kupitia huduma yake ya vifurushi vya  Airtel Yatosha kijulikanancho kama Airtel Jipimie Yatosha Yako itakayowapa wateja wake faida kubwa na uwezo wa kuweza kupanga na kuunda kifurushi wanachokitaka kutokana na chaguo na mahitaji yake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga  alisema "Jiunge sasa na Airtel ufurahie Uhuru huu mpya, Tumezindua " Airtel Jipimie Yatosha Yako " kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu uhuru wa kuchagua na  kupanga matumizi yao na papo hapo kuunda kifurushi  kitakachoweza kukidhi mahitaji yao  ya kiuchumi na kijamii.

Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi ambacho na kinapatikana kwa wateja wetu wote hapa nchini ambapo unaweza kupata kifurushi hiki upendavyo wewe yaani kwa siku, wiki, na  hata mwezi.

“Airte daima tunafanyia bidhaa zetu zote utafiti  na kuziunda kwa mujibu wa kile wateja wetu wanataka ili kuleta unafuu na ubora zaidi, kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa simu za mkononi wa Airtel wataweza kuamua kununua vifurushi vya gharama nafuu na watakavyo vya hadi shilingi  500 huku wakijipimia muda wa maongezi tu, au changanya na MB zaidi au unajichaguali Muda wa maongezi na SMS au kujipimia vyote yaani Muda wa maongezi Zaidi, MB zaidi na SMS Zaidi, uhuru ni wako kujipimia utakavyo” na sasa ndio wakati wa kujiunga na Airte.

Airtel inaamini ubunifu wa huduma ya “Jipimie Yatosha Yako" itakuwa suluhisho la mawasiliano kwa wengi na msaada kwa wale ambao walitaka kifurushi kutokana na hitaji lake. Sasa wateja wa Airtel wanauwezo wa kutengeneza Yatosha yao wao wenyewe  na kutimiza mahitaji yao.

Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga  namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.

Huduma mpya ya uhuru wa kujipimia Vifurushi vya Yatosha imezinduliwa na kusindikizwa na wasanii wa  kundi la Navy kenzo linaloundwa na Nahreel na Haika ambao wataitambulisha sehemu mbalimbali nchini.

“Sisi tuko tayari kama kawaida kuja kujipimia yatosha kila mahali, sasa na nyie kuweni tayari kukamatia chini Yatosha yako inayokutosha" alisema Nahreel wa Navy Kenzo.

No comments: