Tangazo

April 4, 2016

MDUARA UNAPOCHANGANYWA NA RAGGA JIBU NI "KITIMTIM" (VIDEO)

Abraham Mtongole
Muziki unakua sana na hivi karibuni wasanii wengi wa hapa nchini wamekuwa wakibuni mitindo ya aina mbalimbali ili kuzifanya kazi zao ziende mbali na kuvuta mashabiki wa muziki nchini na duniani kwa ujumla. Bayo the Great ni msanii wa kizazi kipya aliyewahi kuvuma na wimbo wa hiphop uitwao Jina Kapuni: https://www.youtube.com/watch?v=qncTaBUAL7E Baada ya ngoma hii Bayo alikaa kimya akifanya shule na baadae kuajiriwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kazi za kijamii kama Solar Aid, The Nature Conservancy, International Citizen Service na Voluntary Service Overseas (VSO) ambako Bayo ameajiriwa mpaka sasa kama Meneja mradi huko Zanzibar.

"Kitimtim" ni wimbo wa mduara wenye vionjo vya ragga uliotayarishwa na producer Mesen Selekta toka studio za De Fatality Dar Es Salaam, video ya Kitimtim ambayo ina comedy story ndani yake imetayarishwa na kampuni ya Focus Films chini ya Nick Dizzo. Unaweza kumsapoti Bayo kwa kutazama hapa chini na kushare wimbo huu na wengine.
Bayo The Great anapatikana kwenye akaunti za mitandao ya kijamii kupitia anuani zifuatazo hapa chini
Twitter: @bayothegreat
Instagram: @bayothegreat
Facebook: Abraham Bayo

No comments: