Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, Salimu Juma Mavaga (kushoto), akizungumza wakati wa kupokea vizimbuzi 'ving'amuzi' vya Kampuni ya StarTimes vilivyo tolewa kwa gharama ya sh,50,000 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Yombo, Chasimba na Maimbwa wilayani humo jana.
Bibi Maendeleo ya Ustawi wa Jamii wa Kata hiyo, Melitha Kiwanga akizungumza katika mkutano huo wakati akiishukuru kampuni ya StarTimes kuwapelekea vizimbuzi hivyo.
Meneja Mauzo wa StarTimes, Tanzania, Tang Jing Yu akizungumza katika mkutano huo kuhusu ugawaji wa vizimbuzi hivyo na nia ya Rais wa China ya kusaidia nchi za Afrika katika mfumo wa mawasiliano wa Kidigitali.
Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa wa Idara ya Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Mayala.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba, akizungumza kwenye mkutano huo wakati akiishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo na kwenda kufungiwa.
Wakina mama wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba (kushoto), akimshukuru Meneja Mauzo wa StarTimes, Tang Jing Yu kwa kuwapelekea huduma hiyo ya vizimbuzi katika karafa yao.
Mwalimu Hilda Stambuli wa Shule ya Msingi ya Yombo akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Tang Jing Yu (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah (wa pili kulia), Kizimbuzi na Dishi lake baada ya kulipia sh.50,000 katika hafla iliyofanyika Kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Juma Mavaga na Fundi Mkuu wa StarTimes Michael Mkufya.
Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kata ya Yombo, Ramadhan Kibwana Shomari (wa pili kulia), baada ya kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa StarTimes, Michael Mkufya.
Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi wa Kijiji cha Chasimba,Miraj Mukadase (wa pili kulia), baada ya kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu wa StarTimes, Michael Mkufya.
Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah akisaini fomu za malipo kabla ya kukabidhiwa kizimbuzi chake pamoja na Dish. Kulia ni Ofisa Idara ya Mauzo wa StarTimes, Joanna Nuhu.
Wananchi wakisubiri kulipia vizambuzi kabla ya kwenda kufungiwa.
Walimu wa Shule ya Msingi ya Yombo wakiwa na madishi yao wakienda kufungiwa baada ya kulipia.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Vizimbuzi ya StarTimes Tanzania imetoa vizimbuzi 50 kwa bei ya sh.50,000 kwa vijiji vitatu vya Matimbwa, Chasimba na Yombo vilivyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vizimbuzi hivyo kwa wananchi wa vijiji hivyo, Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Tang Jing Yu alisema lengo lao kubwa ni kusogeza huduma ya kidigitali kwa wananchi.
"Kampuni yetu imejipanga kuhakikisha inasaidia watu wa vijijini kupata huduma nzuri na kuwanufaisha katika mfumo wa kidigitali" alisema Jing Yu.
Jing Yu alisema kwa awamu ya kwanza wameanza kwa kusambaza vizimbuzi 50 chini ya mradi huo katika vijiji hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wao wa China za kusaidia nchi za Afrika kidigitali hasa katika maeneo ya vijijini.
Alisema China inajisikia fahari kubwa kuona wananchi wa Afrika wananufaika na mradi huo na kwa hapa Tanzania wameanza katika eneo hilo la Bagamoyo lakini lengo likiwa ni kuvifikia vijiji vingi zaidi.
Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala alisema kabla ya kuanza mradi huo waliwatembea wananchi na kuzungumza nao na kujionea changamoto kubwa ya kukosa mawasiliano hayo ya kidigitali.
Alisema kampuni hiyo imetoa vizimbuzi hivyo kwa watu 50 wa vijiji hivyo ambapo watatumia kwa kipindi cha mwezi mmoja bila ya kulipia na amewataka wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo Rashid Kiwamba alisema kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu ni fursa kwao hasa katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia ambapo dunia imekuwa ni kijiji kimoja.
Kiwamba alisema kwamba mradi huo uliopelekwa na StarTimes ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk.John Magufuli aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu za kuhahikisha huduma mbalimbali zinawafikia wananchi ikiwa ni pamoja na mawasiliano.
"Mradi huu tulioletewa na hawa ndugu zetu wa StarTimes ni mzuri na ni mwanzo mzuri na mambo mengi mazuri yanakuja hapa kwetu Yombo ni muhimu wananchi kuuchangamkia" alisema Kawamba.
Mkazi wa Kijiji cha Chasimba Miraj Mukadase aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwapelekea mradi huo ambao utawasaidia kupata taarifa mbalimbali kwa wakati.
"Tulikuwa tukikosa taarifa mbalimbali kwa kuwa tulishindwa kupata vizimbuzi vya bei nafuu na vilivyobora ambapo vilikuwa vikuzwa hadi sh.120, 000 lakini leo hii StarTimes wametukomboa tunawapongeza sana" alisema Mukadase.
No comments:
Post a Comment