Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars
Afrika, Nalimi Mayunga akirekodi video yake na mwanamuziki nguli wa miondoko ya
R& B Akon nchini Marekani.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music
Stars Afrika, Nalimi Mayunga anategemea kuzindua video yake mpya
ijulikanacho kama “Please don’t go away” aliyoifanya na mwanamuziki nguli
duniani Akon nchini Marekani
Nalimi Mayunga alipata nafasi
ya kurekodi wimbo huo mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace
Music Stars Afrika na kuwashinda washiriki wengi kutoka nchi 12
barani Afrika
Kibao hicho chenye mahadhari
ya R& B kimeanza kupigwa au
kuchezwa leo katika radio mbalimbali nchini wakati ambapo video yake
inategemewa kuzinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 20 Mei 2016 wakati wa finali za
msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Star 2016 linalowashirikisha washindi
watano bora ambao wanashindania kitita cha shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja
na nafasi kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AfrikaAirtel Trace Star
yatakayofanyika hivi karibuni nchini Nigeria
Akiongea kuhusu wimbo wake na
Akon, Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga
alisema “ kwa kweli namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa
lakini pia nawashukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii kubwa ya kuweza kurekodi
wimbo na Mwanamuziki wa kimataifa Akon. Nafurahi sana sasa video hii iko tayari
baada ya mashabiki wangu kuisubiri kwa muda mrefu. Natumaini nyimbo yangu
itafanya vizuri ndani na nje ya nchi na kunipa fursa ya kuwa mwanamuziki nyota
na hii ndio imekuwa ndoto yangu. Nawaomba watanzania waniunge mkono ili nyimbo
zangu na muziki wangu uendelee kufanya vizuri.”
Aliongeza kwa kusema ”Napenda pia kuchukua
nafasi hii kuwapongeza washiriki wa mwaka huu walioingia tano bora na
kuwashauri waweke juhudi na nia ili waweze kujinyakulia ushindi na hatimae
kutuwakilisha vyema katika mashindano ya Afrika na kurudi na ushindi nyumbani”.
Aliongeza Mayunga
Naye Meneja uhusiano wa Airtel
Bwana Jackson Mmbando alisema , tunajivunia kuendelea kuwawezesha watanzania
kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi kupitia shindano hili la Airtel
Trace Music Stars.
Tunaamini video ya Mayunga itafanya
vizuri ikiwa watanzania tutamuunga mkono Star wetu huyu, nachukua
fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki kuisikiliza
na kuipiga katika vyombo mbalilmbali kama radio, TV na klabu za muziki ili
iwafikie mashabiki wengi”
Kufatia ushindi wake Nalimi
Mayunga ameweza kupata mafunzo ya muziki toka kwa Akon pamoja na kurekodi kibao
hicho kipya cha “Please don’t go away” na pia amepata nafasi ya kurekodi upya
wimbo wake nchini South Afrika ujulikanao kama “Nice Couple”ambao unaendelea kufanya
vizuri sana kwa sasa.
No comments:
Post a Comment