Tangazo

May 23, 2016

Melisa John Aibuka Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiimba mara baada ya kutangazwa mshindi katika fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars  zilizofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Melisa amejishindia shilingi milioni 50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika. Mshindi wa pili wa mashindano hayo ni  Nandi Charles na Watatu ni Salim Mlindila

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama,  wakati wa fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi Gabriel Kaisi (kulia) akimkabithi Nandi Charles mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, katika shindano hilo Melisa John aliibuka kuwa mshindi wa kwanza.
Mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi na  kukabithiwa mfano wa hundi ya shilingi miliioni 50. Kulia ni mama yake Melisa John,na kushoto nao MC wa fainali hizo.
Mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John akipongezwa na mama yake baada ya kuibuka mshindi nakupata kitita cha shilingi milioni 50.
Majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, Luciano Gadie Tsere (kushoto) na Tony Joett wakifatilia kwa makini washiriki wanavyoimba ili kupata mshindi wa shindano hilo kwa Tanzania. 
Mshindi wa tatu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Salim Mlindila akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Tabasamu, Lucy Ngongoseke.
Baadhi wa waalikwa waliojitokeza kushuhudia shindano la Airtel Trace music Stars wakiwa katika picha wakati wa kokutaili kabla ya shindano hilo kuanza.
Washiriki walioingia katika tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa finali za shindano hilo.

 Wageni waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani  huku akirekodikumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mkononi
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM

Mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya taifa  yamefikia mwisho ambapo Melisa John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam.

Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki wakimarekani Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2.

Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2.

Kufatia ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.

Mshindi wa  Airtel Trace Music Afrika atapata nafasi ya kupata mafunzo ya muziki  na kurekodi video na mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo Keri Hilson , Atlanta nchini Marekani.

“Nimefurahi sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi ndoto zangu. Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini Nigeria.”

Katika fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon.

No comments: