Tangazo

May 5, 2016

NSSF YAZIDI KUZOA WANACHAMA WAPYA


Wananchi wa maeneo ya Banana jijini Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kujiandikisha na kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ambapo jumla ya wanachama 160 walijiandikisha katika eneo hilo. Katika eneo la Mwembeyangawanachama wapya 214 walijiandikisha na Mbagala 132 na kufanya jumla ya wanachama wapya 506 walijiandikisha.
Elimu ikizidi kutolewa kwa wananchi kuhusu Hifadhi ya Jamii.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam akiweka alama ya dole gumba baada ya kujiunga na NSSF.
Wananchi wakiendelea kujiandikisha.
Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akitoa elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa wanachi waliojitokeza katika banda la NSSF.
Wananchi wakisubiri kujiandikisha.
Wananchi wakijiandikisha baada ya kupata elimu ya faida ya kujiunga na NSSF.
Ofisa Uendeshaji wa NSSF, Yusuf Magogo akimsaidia kujaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Nasra Masaka wakati wa kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari iliyofanyika katika eneo la Banana jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wsa maeneo mbalimbali wakijiandisha ili kujiunga na NSSF.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aman Marcel (kulia), akimjazia fomu ya kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, Leonard Kongwa wakati wa kampeni maalumu ya kuelimisha na

kuandikisha wanachama wa Hiari iliyofanyika katika eneo la Banana.

Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akimsaidia kujaza fomu ya mwanachama mpya aliyejiunga na NSFF.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aman Marcel (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fulana, Octavian Deodath mara baada ya kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSS katika eneo la Banana jijini Dar es Salaam. 
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari wakazi wa eneo la Banana jijini Dar es Salaam.

No comments: