Tangazo

May 5, 2016

Tigo 4G LTE yaingia kwenye Miji mitano katika Kanda ya Ziwa


Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa Tigo kusambaza mtandao wa 4G lte nchi nzima pembeni yake ni Afisa Mkuu wa Ufundi wa teknolojia ya mawasiliano wa Tigo Jerome Albou katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakichukua taaarifa


                                Mtandao wa Tigo 4G LTE ni mpana na wa kasi Tanzania

Dar es Salaam, Mei 4, 2016-Kampuni ya simu ya Tigo ambayo inaendesha maisha ya kidijitali Tanzania imetangaza kuzinduliwa kwa  huduma ya 4G LTE katika miji mingine mitano ya kanda ya ambayo  ni Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma na Shinyanga.

 Kampuni hiyo awali ilizindua  huduma hiyo  jijini Dar es Salaam  mwanzoni mwa mwaka jana  na baadaye kuisambaza katika miji ya Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza na hivyo kuifanya  kuwa kampuni ya simu  yenye mtandao mpana na wa kasi  wa 4G LTE nchini Tanzania.
Ikiwa inachukuliwa kuwa ni  teknolojia  nzuri  na  ya uhakika katika sekta ya mawasiliano ya simu duniani ya kupata  intaneti, kasi ya teknolojia ya 4G LTE  ni takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G na Tigo inaifanyia kazi kwa kina ili kuongeza ubora wa huduma hiyo na mtandao wa 4G kutokana na matumizi ya wateja kuwa  nayo yanaongezeka kwa kasi  kubwa.

Hivi sasa Tigo ina timu inayofanya kazi saa zote  kuimarisha na  kukuza ubora wa teknolojia ya 4G. Matokeo yake ni kwamba  mtandao wa 4G umekuwa unategemewa  kwenye miji ambamo upo (Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza).

Mtandao wa 4G LTE unatoa intaneti ya kasi ya kurambaza (surf) na kupakua vitu, kufanya  miito ya simu ya kuonana (Skype)  isiyo na kikomo.  Kutokana na uzinduzi wa hivi karibuni  wa video za bure  kupitia YouTube nyakati za usiku,  mtandao wa 4G LTE unawawezesha wateja kwa kiwango kikubwa  kupata uzoefu wa kutiririsha video zilizo na uangavu mkubwa. Aidha kutokana na ushirikiano na   Facebook mteja wetu wa 4G pia anaweza kufurahia kutiririsha video zilizomo kwenye  mitandao maarufu ya kijamii  duniani.

Pia,  mteja akiwa na  4G LTE  anaweza kupakua mafaili  makubwa  (sinema, mafaili yanayohusiana na kazi) au vifaa  na hali kadhalika kucheza michezo kwa njia ya mtandao.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  leo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez,   alisema  mpango wa kupanua  teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote ya nchi upo mbioni  ambapo kampuni hiyo imejikita kwenye kuwapa wateja wake huduma  zenye ubora  duniani ambazo zitawawezesha  kufurahia  mtindo wa maisha ya kidijitali.

 “Kupanua mtandao wa 4G LTE nchi nnzima  kwa mara nyingine kunaonesha sio tu Tigo kuongoza  kwenye kutoa  teknolojia  na ubunifu wa kisasa  ndani ya soko  bali pia kusisitizia  kujituma kwetu  katika kuongeza fursa ya kufikia  intaneti kwa Watanzania walio  wengi kwa kadri iwezekanavyo,’ alisema Gutierrez.

Kwa mwaka huu 2016,  Tigo itawekeza  zaidi ya dola milioni 75 kwenye upanuzi wa mtandao na kuimarisha ubora wake kwa  kukuza maeneo ya teknolojia ya 4G na 3G, mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya sehemu za kutolea  huduma kwa wateja  nchi nzima.

 “Tukiwa kama kampuni tunatambua  umuhimu wa  wa ubora na ukaribu  kwa wateja wetu na tunafanya kazi  ili kufikia malengo hayo katika siku za karibuni,” alisema Gutierrez.

 “Hivi sasa pia tuna programu ya kufanya mtandao  kuwa wa kisasa ambao unajumuisha  kuongeza  uwezo wa 4G  kwenye miji yote 12 ambako tuna mtandao wa 4G  pamoja na kuongeza  mtandao wa 3G kufika maeneo yote nchini,” alisema Gutierrez  na kuongeza kuwa wateja wa Tigo  katika miji ya Mbeya, Mtwara na Lindi  wajitayarishe  kufurahia  huduma ya Tigo 4G LTE  itakayoanza kutolewa  siku za hivi karibuni.

No comments: