Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (wa pili
kulia) wakijipongeza kwa pamoja na washiriki waliochaguliwa kuingia tano bora
katika shindano la Airtel Trace Music Stars ambapo fainali zake
zitakafanyika tarehe 20 mei 2016 hapa jijini Dar es Saalam. Mshindi ataondoka
na zawadi ya shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika
mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria
XXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washiriki waliongia kwenye tano
bora katika shindano kubwa Afrika la kusaka vipaji vya muziki lijulikanalo kama
Airtel Trace Music Stars.
Ikiwa
ni miezi mitatu tangu kuanza kwa msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace
Music Stars na kushirikisha maelfu ya vijana wa kitanzania, Airtel
imetangaza majina ya washiriki wa tano bora walioingia kwenye fainali za
kitaifa ambao ni pamoja na Benny Sule, Nicole Grey, Nandi Charles, Melisa Elina
John na Salim Mlindila.
Washiriki
hawa walichaguliwa na jopo la majaji mahiri akiwemo mtangazaji wa TV
mahiri, Mwanamuzi, Mwigizaji na msanii aliyejikita katika maeneo mengi, Jokate
Urban Mwegelo, mtunzi wa nyimbo na mwalimu wa sauti Tony Joett pamoja na
mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere.
Akitangaza
walioingia tano bora, Afisa Uhusiano wa Airtel , Jane Matinde
aliwapongeza washiriki hao kwa kufika katika hatua ya fainali na kusema “
msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars umekuwa ni wa mafanikio
makubwa na leo tunayo furaha kutangaza majina ya washiriki waliofanya vizuri
zaidi na kuwa kwenye nafasi ya kushinda na kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya Afrika”.
“Tunaamini
Airtel Trace Music Stars ni Fursa muhimu ya kuwainua wanamuziki chipikizi
kuweza kuonyesha vipaji vyao na hatimae kuzifikia ndoto zao. Airtel itaendelea
kuwawezesha vijana wa kitanzania kutambua uwezo wao na kuishi ndoto zao na
shindano hili la Airtel Trace Music Stars ni kielelezo tosha cha dhamira hii”.
Aliongeza Matinde
Kwa
upande wake mmoja ya washiriki waliotinga tano bora , Benny Sule alionyesha
furaha yake ya kufika katika finali na kusema “ mashindano haya yamenipa Fursa
kubwa kiasi ambacho nashindwa kuelezea. Nimejipanga vyema kushiriki katika
fainali zinazofanyika wiki ijayo na natumaini kushinda na kuiwakilisha vyema
nchi yangu
Aliongeza kwa kusema “Huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa
mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi. Nawashukuru sana Airtel kwa mpango huu
ambao umewawezesha vijana wengi barani Afrika kuonyesha vipaji vyao na
kuzifikia ndoto zao.”
Washiriki waliongia tano bora wanategemea kushindana katika
kinyanganyiro cha mshindi wa Airtel Trace Music Stars wa Tanzania katika finali
zitakazofanyika tarehe 20 Mei 2016. Mshindi ataondoka na zawadi ya
shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano
ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria ambapo atapata nafasi ya kushinda na
kusaini mkataba wa mafunzo.
Tunatoa wito kwa watanzania kuwapiigia kura washiriki ili kupata
mshindi atakayetuwakalisha vyema katika mashindano ya Afrika, ili kupiga
kura weka jina la fumbo (nickname) ya mshiriki kisha tuma kwenda namba 15594 .
zifuatazo ni jina la fumbo (nickname ) za washiriki Beny Sulle
“Ben”, Nicole Grey “Nic, Nandi Charles”Nan”,Melissa John “Mel”na Salim Mlindila
“Sal”.
No comments:
Post a Comment