Tangazo

June 20, 2016

VETA na Airtel yapeleka VSOMO DODOMA

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa    akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi  Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma  kupitia simu ya mkononi. 
Wanafunzi wa Chuo cha Veta Dodoma wakifuatilia kwa makini katika uzinduzi huo.
 xxxxxxxxxxxxxxxxx

• Ni mafunzo ya stadi za ufundi kwa njia ya simu za mkononi
 
Dodoma 

VETA wakishirikiana na Airtel kupitia AIRTEL FURSA inaendelea kufanya mafunzo ya stadi za ufundi kuwa katika njia rahisi na nafuu kwa watanzania. Katika  kuhakikisha kwamba vijana wa kitanzania wanafikiwa popote pale walipo, VETA na Airtel wamewasili katika mkoa wa Dodoma na kutoa fursa ya mafuzo ya stadi za ufundi katika mkoa huo.
 
kozi zinazotolewa ni pamoja na ufundi pikipiki, ufundi umeme wa majumbani, ufundi wa simu za mkononi , ufundi Alluminium, utaalamu wa masuala ya urembo na ufudi wa kuchomea vyuma. Kozi zinazotolewa katika awamu hii ya kwanza na VETA kupitia kadi ya simu ya Airtel zinatolewa kwa bei ya chini kabisa ya Sh.120,000/=. Muda wa kujisomea kozi ya vitendo katika chuo cha VETA  baada ya kufaulu kozi ya nadharia ni jumla ya masaa 60 . Hii ikimaanisha kuwa mtu atakayeweka msimamo na kusoma kwa bidii ataweza kumaliza ndani ya mwezi mmoja na kuweza kupata cheti chake.
 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa alitoa maoni yake juu ya mafunzo yanayotolewa na VETA kupitia Airtel, alisema, "Nafurahi kwamba VSOMO imekuwa si tu kwa kuwa bei nafuu lakini pia urahisi wanaoupata vijana kwani wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku kama wameajiriwa na kuboresha ujuzi wao kupitia mtandao pale wanapopata nafasi. Naona wasichana wengi sasa wataweza kupata ujuzi wa kupika kwa kupitia simu  zao za mkononi.

Akitoa maoni yake juu VSOMO, Mkuu wa chuo cha Veta Kipawa Dar Es Salaam, Eng. Lucius Luteganya alisema, "Tunaamini mpango wa VSOMO utabadilisha mtazamo wa vijana wetu na kutumia zaidi teknolojia na kusoma kupitia mitandao.
 
Amewahimiza vijana wa Dodoma na mikoa ya karibu kutumia VSOMO kama fursa ya kuongeza ujuzi ambao unahitajika katika soko hili gumu la ajira. “Tunafuraha kubwa sana na mpango huu ambao Veta wameweza kuuungana na Airtel kwa kuweza kubadilisha maisha ya vijana wa kitanzania".

Hii ni wiki ya pili toka kuanzishwa kwa VSOMO ambapo vijana wa Dodoma walishiriki katika warsha ya kujiunga na VSOMO mwishoni mwa wiki hii, ambapo vijana wengi walijitokeza na kujiunga na masomo haya ya VSOMO. VSOMO  ni mafunzo ya stadi ya ufundi kwa njia ya mtandao kwa wateja wa Airtel wenye simu za aina ya android, ambapo mteja  anatakiwa kupakua VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kulipa  gharama ya sh 120,000 / = tu.

No comments: