Tangazo

July 18, 2016

Airtel yasaidia wadau wa Elimu, Afya na Kilimo mkoani Tabora

Ayub Kim, Mraditi wa kitengo cha miundo mbinu Milllenium Promise Tanzania,  akitoa mafunzo ya komputa kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolangulu mkoani Tabora, wanafunzi hawa wamewezesha huduma za mawasiliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wa millennium village

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

·Kupitia mradi wake wa Millinium village 
·Wanafunzi , huduma na wakulima waunganishwa huduma za internet bure ili kupata taarifa mbalimbali

Wahudumu wa sekta mbalimbali za kijamii wilayani Uyui Mkoani Tabora na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ilolangulu mkoani humo wameanza kunufaika na mradi wa Millenium Village unaowawezesha kuunganishwa na kujifunza kupitia wa mtandao wa Airtel  kwa huduma za Internet na za simu ya bila malipo.

Hayo yamebainishwa na Wahudumu wa sekta za Elimu, Afya, maji na Kilimo baada ya  Kampuni ya simu za mkononi Airtel kuwapatia msaada wa laini  za simu  na kuwaunganisha kwenye huduma za internet na kupiga simu bila malipo yoyote. Mradi wa millium village ulianza toka mwaka 2013 kwa lengo la kuwawezesha watoa huduma waishio vijijini kukusanya takwimu za kila mwezi kwa njia ya mtandao, kupatiana taarifa za utekelezaji wa kazi zao na kuwafikia wanufaika kwa urahisi

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wahudumu wa sekta hizo wamesema wameendelea kunufaika huduma za Airtel chini ya mradi  huo na kuzitumia vyema katika utekelezaji wa kazi zao

“mpango huu umeturahisishia kutoa huduma za afya kwa jamii ya mbola hususani kwa wamama wajawazito na watoto kwani tunapowatembelea majumbani mwao tunaweza kuwasaidia kwa kuwasiliana na wenzetu kirahisi na pia kuchukua takwimu zao na kuziweka kwenye application maalumu ijulikanayo kama CommCare Application na taarifa zao zinasomeka kirahisi na kwa wakati katika vituo vyetu vya afya.  tunashukuru sana Airtel kutupatia huduma hizi bure kwani mawasiliano ya simu ni muhimu sana na yanachochea kuwa na jamii yenye afya bora  kwani toka mwaka 2013 hapa mbola hatujawahi kuwa na kifo cha mama mjamzito na mtoto mchanga alisema Mhudumu mkuu wa afya vijijini katika cluster ya ndola , Charles Masanja”

Naye Kaimu mkuu wa shule ya Ilolangulu,  Jumanne Mailani amesema kupitia mtandao wa Airtel na chini ya mradi wa (Airtel Connect to lean)  Wanafunzi wanauwezo wa kupata taarifa mbali mbali za kimasomo kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo kuongeza uelewa na ufaulu shuleni hapo. Lakini pia wanafunzi wetu wanapata fursa ya kujifunza masomo ya komputa na kuunganishwa na huduma za internet na kupata nyenzo zaidi zinazowaongezea maarifa katika masomo yao.

Kwa upande wake Ayub Kim , Mraditi wa kitengo cha miundo mbinu Milllenium Promise Tanzania alisema “Tunashukuru sana Airtel  kwa kushirikiana nasi kupitia program hii ya Milllenium Village ambapo mpaka sasa huduma za Airtel zimekuwa msaada mkubwa katika kuendesha huduma mbalimbali hapa mbola na kuwafikia wakazi zaidi ya 45,000. Tumeanzisha Saccos yetu ambayo pia inaendeshwa kwa kutumia mtandao wa bure wa internet na simu kutoka Airtel na pia tumepata mavuno mengi sana toka kwa wakulima kwani tunaowatoa huduma ambao wanatoa elimu kwa wakulima ili kuinua kilimo chao. Kwakweli tumepata mafanikio makubwa kwani tunawawezesha watoa huduma katika sekta mbalimbali kama vile , kifedha, kilimo,elimu , maji na afya kunufaika na huduma hizi za mawasiliano za Airtel na kuongeza ufanisi zaidi.

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Airtel support health, agriculture and education stakeholders in Tabora

·Through Millennium Village project
·Student, health workers and farmers are connected to free mobile service for easy access of information

Workers in various sectors at uyui district in Tabora region and student form Ilolungulu secondary in the region have benefited from Millennium village project which enabled learning and connecting to the internet services through Airtel mobile communication services at no cost

This has been notified by workers in education, health, agriculture sector following Airtel support in provisioning of mobile simcard with free talk time and internet bundles to performer their duties.  In 2013 Airtel through Millenium village project donate this aid with the purpose of facilitating workers in remote areas accumulate data online, access information online in order to reach out to the community effectively

Speaking about the program Charles John Masanja,  Senior Social Health Worker in ndola Cluster said” this program has simplified health services in mbola, we are now able to attend to emergency, assist patient at home especial pregnant women and babies by communicating to our colleagues while in the field for further support. We have also managed to collect patients’ data and upload them in our application called “CommCare Application” to be viewed by staff in health centers on real time.  We thank Airtel for this support as communication is key in nurturing a health community

In his part, Assistant head master for Ilolungulu Secondary school, Jumanne Mailani said” through Airtel services and under the project dubbed “Airtel Connect to Lear” student from the school communicate and share information through the use of Skype programme with students from New Canaan School which has enhance the school performance. Teachers and students are benefiting a lot through the use of internet to search materials and for email communication purposes. Additional our student are now taught computer courses and acquire necessary ICT skills at ordinary level

On his side The Millennium promise Tanzania iCT, E-health specialist, Ayub Kim said” we started this program 2013 and today we are witnessing lots of success,  various sectors including health, water , financial institution (saccos) education and agriculture are all connected to Airtel services and offer their services in more efficient manner.  As it  is in health sector we also deploy Agriculture  Community Workers to support farmer in their agricultural activities, they have seen a significant increase of production each year. We thank Airtel for partnering with us to enable more than 4500 in mbola  Tabora  benefit from quality services powered by Airtel communication tower.


No comments: