Tangazo

July 18, 2016

TWIGA CEMENT KUGAWA BURE MIFUKO 4,800 YA SARUJI KWA WATEJA WAKE

Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Tanzania Portland Cement Ltd, Simon Delens akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya kampuni ijulikanayo kama “Jijenge na Twiga Cement” , ambapo jumla ya mifuko 4,800 ya saruji itashindaniwa. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Martha Haule.
XXXXXXXXXXXXXXXX
DA

Wateja wa Tanzania Portland Cement Company Ltd (TPCC), wazalishaji wa brandi ya ‘Twiga Cement’ watapata nafasi ya kushinda mpaka mifuko 4,800 ya cement, mashine 2 za kufyatulia matofali na mixers kwenye droo ya kitaifa.

Tanzania Portland Cement Company Ltd, kampuni inayoongoza kwenye soko la cement nchini, imetangaza uzinduzi wa ‘Promosheni ya Jijenge Na Twiga Cement ’, ili kuwazawadia wateja wake waaminifu.

Washindi wa promosheni ya Jijenge na Twiga Cement watapata nafasi ya kushinda hadi mifuko 600 ya cement, kampuni imetenga jumla ya mifuko 4,800 ya cement kwaajili ya promosheni hii. Zawadi zinginezo ni mashine za kufyatulia matofali, mixers, matoroli na zawadi nyingine kibao.

Yafuatayo hapo chini ni mambo muhimu yakuzingatia kwa washiriki wote:

Promosheni itaendeshwa ndani ya wiki 4, kuanzia tarehe 18 July   2016 mpaka Tarehe 12th  Agosti  2016.

Promosheni imeundwa kwa mfumo wa ‘droo, ambapo washindi watakuwa wanatangazwa kila wiki (kila Ijumaa asubuhi).

Mteja yeyote wa Twiga Cement atakaye nunua  mfuko wa Twiga Cement Extra ana haki ya kushiriki.

Namba maalum ya siri (tarakimu na herufi) imewekwa kwenye valvu ya kila mfuko wa Twiga Cement utakaonunuliwa.

Maelekezo ya jinsi ya kuipata na kuitumia namba ya siri utayapata juu ya kila mfuko wa cement.

Kushiriki, Tuma hiyo namba maalum ya siri uliyopata kwenda 0789 000 666, na utakuwa umeingia kwenye droo ya wiki.

Promosheni ya Jijenge Na Twiga Cement itakuwa na jumla ya washindi 114.

Wateja wanaweza kushinda mpaka mifuko 600 ya cement ikiwemo pia na zawadi nyingine zilizotajwa na vifaa.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ‘Promosheni ya Jijenge Na Twiga
    Cement’ mkurugenzi wa Masoko  Mr. Simon Delens, alisema promosheni ya kipekee kama hii haijawahi kufanywa na kampuni nyingine yoyote ya uzalishaji wa cement nchini, na leo, Twiga Cement inajivunia kuzindua promosheni hii ya kipekee ambayo inawahusu wateja wote wa Twiga Cement nchini.

Mr. Delens alimalizia kwa kuwakumbusha na kuwahamasisha wateja wa Twiga cement waendelee kutumia brandi ya Twiga Cement, huku wakifurahia faida zinazowajia kwakuwa wadau mahiri. Huu ni mwanzo tu wa safari nzuri na kubwa sana, na pia programu nyingine kibao zinakuja mwaka huu.

Kumbuka:

1.    Washindi wote watapigiwa simu kutoka ofisi za Twiga Cement kwenye namba 0785 670 669, kuwapa taarifa ya siku na jinsi ya kuchukua zawadi.

2.   Washindi wote ni lazima wawasilishe valvu ya ushindi iliwaweze kupokea zawadi zao.

3. Washindi wa nje ya Dar es Salaam watatakiwa kuripoti kwa wasambazaji wetu waliochaguliwa kuchukua zawadi zao.

4. Siku ya mwisho ya kudai zawadi katika makundi yote ni Tarehe 12th September 2016.

5. TPCC haita gharamia gharama zozote za usafiri kwa mshindi wakati wakukuchukua zawadi.

No comments: