Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho 23 ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Sehemu ya Wakazi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Luteni Joseph Benedict Lyakurwa wa Suma JKT
alipotembelea eneo lao na kujionea shughuli mbali mbali za kilimo na
ufugaji kwenye kilele cha maadhimisho ya 23 ya sikukuu ya wakulima ya
Nanenane mkoani Lindi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka
kwa Afisa Kilimo Daraja la kwanza Halima Kikwega wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane , Ngongo Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi mikono wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya Wakulima Nane nane mkoani Lindi.
...............................................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati
ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana
na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo
ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya
maendeleo ya wananchi.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya
sikukuu ya Wakulima Nane Nane kitaifa katika uwanja wa Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani Lindi kwa naiba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika
hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Ngongo, Makamu
wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo
tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa
wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama
hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.
“Napenda kuwahakikishia kuwa tuna
dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za
kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini
au itikadi za vyama vyenu.”
Kuhusu
uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan amesema maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane ni moja katika ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi
katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo
na uvuvi kote nchini.
Amesisitiza
kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na
kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika
kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Makamu
wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga
kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta
makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha
2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi
asilimia 12.
Aidha
amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka
3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua
mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la
Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.
Kwa
Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amehimiza wananchi kote
nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi
ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa
mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza
pato la familia na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment