Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Kongamano la Pili na Maonesho ya Kitengo cha Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
Sehemu ya Waandishi waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Steven Mlote akihutubia kwenye Kongamano hilo la Wahandisi Wanawake.
Mwakilishi wa Balozi wa Norway akihutubia kwenye Kongamano hilo la Wahandisi Wanawake lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan aonyesha zawadi ya Saa aliopewa na Wahandishi Wanawake (TAWESE) kwenye Kongamano la Pili na Maonesho ya Kitengo cha
Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mhandisi Mshauri Bi. Warda Ester Mash'mark alipotembelea banda lake wakati wa Kongamano la Pili na Maonesho ya Kitengo cha
Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Anifa chingumbe wa TTCL namna ambavyo mtandao wa 4G LTE unavyofanyakazi alipotembelea banda la TTCL kwenye Kongamano la Pili na Maonesho ya Kitengo cha
Wahandisi Wanawake cha Taasisi ya Waandisi Tanzania.
..........................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewataka wahandisi wanawake nchini kufanya kampeni maalum ya kushawishi watoto wa kike kujenga ari ya kusoma masomo ya sayansi na hisabati kama hatua ya kuongeza maradufu wahandisi wanawake nchini.
amewataka wahandisi wanawake nchini kufanya kampeni maalum ya kushawishi watoto wa kike kujenga ari ya kusoma masomo ya sayansi na hisabati kama hatua ya kuongeza maradufu wahandisi wanawake nchini.
Makamu Rais ametoa kauli hiyo 12-Aug-16 wakati anafungua kongamano la
maonyesho ya kitengo cha wahandisi wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesisitiza
kuwa kampeni hiyo itasaidia kuelimisha wasichana,kuwaunganisha na kuwaendeleza
watoto wa kike ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuchangia
maendeleo ya nchi kupitia fani za sayansi na teknolojia.
Makamu wa
Rais amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa wahandisi katika maendeleo
ya nchi hususani katika sekta za nishati,madini,barabara,maji, uvuvi na kilimo
imeendelea kuweka mipango madhubuti ya kuinua na kuimarisha fani ya uhandisi
hapa nchini.
Ameeleza
kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuongeza vyuo vya uhandisi
kutoka chuo Kimoja mwaka 1970 mpaka vyuo Tisa hivi sasa na kuongeza maabara katika
shule za umma ili kuwavutia wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan pia amepongeza baadhi ya halmashauri nchi ambazo
zimekamilisha ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari na kuweka vifaa vyote
vya kujifunzia.
Kuhusu
wakandarasi wa ndani ya nchi, Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kuwapa
kipaumbele wakandarasi wazawa wenye
uwezo katika ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kuwajengea
uwezo.
Amesisitiza
kuwa matumizi ya wakandarasi wazawa wenye uwezo wa kufanya kazi yatasaidia kwa
kiasi kikubwa kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania kuliko kutumia
wakandarasi wa nje ambao mara nyingi baadhi yao wanaajiri watalaamu kutoka
kwenye nchi wanazotoka kuliko kuajiri
Wataalamu wa hapa nchini.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameshauri Taasisi ya Wahandisi Tanzania iendelee na jukumu
la kuwaunganisha wahandisi wote watanzania ndani na nje ya nchi kwa manufaa ya
taifa na ameishukuru serikali ya Norway kwa mchango wao wa shilingi bilioni 4.3
ili kuchangia mpango wa miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi 2021 ambao
utasaidia kuwajengea uzoefu wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa na bodi ya
usajili ya wahandisi nchini.
Makamu wa
Rais amesema mpango huo pia unatarajiwa kunufaisha wanafunzi wa kike 150 nchini
na utaisaidia serikali kufanikisha lengo la kufikia uchumi wa viwanda na kipato
cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella
Manyanya ameiomba serikali ihakikishe inakamilisha mpango wa kuweka vifaa
kwenye maabara za shule za sekondari kote nchini kama hatua ya kuwavutia
wasichana wengi kusoma masomo ya sayansi.
Kulingana na
takwimu za Kitengo cha Taasisi ya Wahandisi Wanawake Tanzania idadi ya
wahandisi wanawake imeongezeka kutoka wanawake 35 mwaka 2005 hadi wanawake wahandisi
298 mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment