Tangazo

August 29, 2016

YANGA YAANZA KWA KISHINDO LIGI KUU, YAIBURUZA AFRICA LYON KWA BAO 3-0



MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza vizuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, viungo Deus David Kaseke aliyefungua pazia  kipindi cha kwanza, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Rajab Mrope wa Ruvuma, Mirambo Tshikungu wa Mbeya na Janeth Balama wa Iringa, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Kaseke dakika ya 18, akimalizia pasi ya winga Simon Msuva, ambaye leo alikuwa katika kiwango chake.


 Donald Ngoma wa Timu ya Yanga (jezi 11) katikati akijaribu kuwatoka mabeki ya Lyon, kulia ni Abdul Hilary na namba 26 mgongoni ni Amani Peter



 Wanachama wa Timu ya Yanga wakimpungia mikono SimonMsuva
 Simon Msuva, akiwapungia mikono wanachama na wapenzi waliokuwa wakimpungia mikono katika Uwanja wa Mpira wa Taifa



 Mchezo ulianzia hapa  kutoka kwa Harun Niyonzima kwa kmpatia pasi Simon Msuva kwa kupachika mpira katika nyavu za goli la Afikan Lyon, angalia picha tatu za chini na kufanikiwa kumtoka Kipa wa Lyon
 Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa katikati akimtoka Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand
 Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa katikati akimtoka, Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand
  Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa kulia  akimtoka, Omar Salum na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand, hapa mlinda mlango akishuhudia kwa macho mpira unavyo tinga golini, mpira uliopigwa kwa kicha na  Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu  Tanzania Bara, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
   Simon Msuva kulia akifurahi baada ya kuipatia timu yake goli akiwa na Juma Mahadhi
 Donald Ngoma akiwana Mpira

Wanachama wa Timu ya Simba wakiwa na butwaa kutoamini kinacho tokea Uwanjani hapo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments: