Tangazo

September 19, 2016

Airtel na Mhealth Tanzania kuendelea kusaidia wanawake Tanzania

Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi
·  Zaidi ya wateja wa Airtel 350,000 wanufaika na mpango wa Wazazi Nipendeni
Airtel Tanzania yajivunia kufikia ujumbe mfupi (sms) upatao 20,0000 bila gharama yoyote kwa wateja zaidi ya 350,000 kwa ushirikiano na mHealth  Tanzania kupitia huduma yao ya Wazazi Nipendeni (Afya ya uzazi na mtoto) tangu kuzinduliwa 2012. Wateja wa Airtel waliojiunga na huduma hii wamekuwa wakipokea ujumbe mfupi wa bure wenye taarifa muhimu za afya na kupata ushauri kwa wamama wajawazito na wenye watoto wadogo Tanzania nzima.
Kubainisha hayo Mama lishe Aneth Pius (30) kutoka Dar es Salaam alisema, “ninamimba ya miezi 7 na nimekuwa napata ujumbe mfupi wa tarehe za kutembelea zahanati na umuhimu wa kufanya maadalizi mapema kabla ya kujifungua na pia athari za kutojiandaa unapokaribia kujifungua. Naishukuru sana Airtel na mHealth kwa huduma hii inayonisaidia katika kipindi hiki cha ujauzito”.
Miongoni mwa wateja 350,000 wa Airtel waliojiunga na huduma hii, 31% ni wanawake wajawazito, 18% ni wazazi wenye watoto wachanga, 17% ni wasaidizi wa afya na 34% ni wateja waliojiunga kupata taarifa mbalimbali za afya.
Akizungumzia hilo, Meneja huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi  alisema, “Airtel inajivunia kuwa kampuni ya simu ya kwanza kushirikiana na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika mpango wa Wazazi Nipendeni (Afya uzazi na mtoto) uliozinduliwa 2012. Kutokana na kuenea kwa mtandao wetu nchi nzima na wateja zaidi ya million 11 tulitambua umuhimu wetu katika kuwezesha upatikanaji wa taarifa za afya kwa jamii”.
Bayumi aliongezea akisema tunatamani kuona watu zaidi wakinufaika na huduma hii kupitia mtandao wetu na tunaendelea kuhakikisha tunatoa huduma hii bure kabisa kwa wateja wetu nchi nzima.
Huduma hii inasimamiwa na mHealth Tanzania ikishirikiana na washirika mbalimbali duniani. Njia ya kutoa taarifa za afya kwa ujumbe mfupi (SMS) imetambuliwa kuwa moja ya huduma bora nne za kutoa taarifa za afya duniani kwa mwaka 2014 na GSMA , Global Mobile Awards Committee, na moja kati ya huduma 6 zitokanazo na ubunifu wa kimtandao kwa 2016 na GSMA , Global Mobile Awards Committee.

No comments: