Tangazo

October 27, 2016

DC HAPI KUFUNGUA MAONESHO YA KWANZA YA WAJASILIAMALI WA AIRTEL FURSA

Moja kati ya wajasiriamali watakaokuwepo katika maonyesho ya wajasiriamali ya Airtel FURSA, Bi. Theresia Maliatabu akiandaa bidhaa zake za picha za Sanaa nyumbani kwake mbagala rangi tatu. Theresia ni moja kati ya wafanyafanya biashara waliowezeshwa na mradi wa kuinua vijana wa  Airtel FURSA

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 DAR ES SALAAM

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi anatarajiwa kufungua maonyesho ya wajasiliamali mbalimbali wanaodhaminiwa na Mpango wa Airtel FURSA yatakayofanyika ijumaa hii  katika viwanja vya ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.

Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA tunakuwezesha, umeandaa mpango utakaowawezesha wajasiriamali  hao ambao awali waliowazezwa kupitia mpango wake wa Airtel FURSA ili waweze kuonyesha biashara zao kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara  kutangaza na kupata masoko ya biashara zao  ili kukuza biashara na mitaji yao.

Akiongea juu ya maonyesho hayo, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “ tumeonelea ni vyema kujipanga katika kuendeleza dhamira yetu ya kuwainua vijana na kuhakikisha mpango huu wa Airtel FURSA unaleta tija na kuinua biashara zao. Watakaoshiriki ni  zaidi ya wafanyabiashara 28 na vikundi vinne vilivyonufaika kwa  kupatiwa vitendea kazi kupitia mradi wetu wa Airtel FURSA ambao kwa sasa wanafanya vizuri katika biashara zao”.

Airtel tumeona ni vyema tukiendelea kuwawezesha kwa kuwatafutia masoko endelevu ndani na nje ya nchi kwa kuwashirikisha katika maonyesho haya yenye lengo la kutangaza biashara zao na kupata masoko zaidi, tunatoa wito kwa watanzania kuwaunga mkono kwa kufatilia kazi zao kupitia mitandao ya kijamii na kupata fursa ya kutembelea maonyesho haya siku ya kesho.

Bidhaa zitakazo kuwepo katika maonyesho hayo ni pamoja na Sanaa za picha za ukutani, vifaa vya magari, vyakula mbalimbali kama matunda ,korosho, cake, mifugo kama vile kuku wa kisasa,  bidhaa za kiafrika, mapambo ya nyumbani na kadhalika.

No comments: