Tangazo

November 30, 2016

MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA KAMPUNI YA MASOKO YA KISMATY ADVERT MEDIA



Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company Ltd, Bi. Mary Emmanuel Mollel akizungumza Machache katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.

Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd Mary Emmanuel ,akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro , mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Co. Ltd, Bi. Mary Emmanuel ,na Mratibu wa shughuli hiyo Bi. Dotto Kimaro katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Mchekeshaji 'Steve Nyerere' nae hakubakia nyuma alikuwepo akifanya yake katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.

Watatu kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Calist Lazaro ,Naibu meya Bi. Viola Lazaro ,Diwani wa kata ya Themi Kinabo na Diwani wa kata ya Levolosi Ephata Nanyaro katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Wa pili Kutoka Kushoto ni Meneja wa Venus Hotel Mr. Prashant akiongozana na mkewe na rafiki yao Mr. Dibin wakiwa katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.

Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company Ltd, Mary Mollel akikata keki kwa kushirikiana na Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Calist Lazaro, katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.


Keki ya ndafu nayo ilihusika sana kwa ukaribu, katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.



Mambo haya nayo hayakosekaniki katika hafla kama hii shampein ikifunguliwa hapa na  mmoja wa waandishi wa habari wa kituo cha TV jijini Arusha Millan Cable Hamza Kalemela ,pamoja na mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mwananchi communication Zulfa Musa katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.Mambo yakiendelea kama uonavyo hapo pichani, 
katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.
Afisa uhusiano  wa Kismaty Advert Media  Company Ltd ,Bw. Gadiola Emmanuel akipongezana na Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media company ltd Bi. Mary Emmanuel Mollel ,katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016. Cheers !Wakiwa wanapongezana, Glass Juu Hewani...kuashiria Amani na Furaha katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Meya wa Jiji la Arusha amesema kuwa ni vyema kusapoti na kuyapa kipaumbele mambo mazuri yanayofanyawa na wazawa haswa kwa uthubutu wao wa kufanya mambo ya maendeleo.

Aliyasema hayo katika uzinduzi wa kampuni ya matangazo inayojulikana kama Kismaty Advert Media company ltd , iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Asili Resort uliopo Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini.
Meya huyo amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutangaza biashara zao kwani bila kufanya hivyo hata kama bidhaa itakuwa na uzuri kiasi gani hakuna atakayefahamu thamani yake bila kuitangaza ndipo ifahamaike.

"Jengeni tabia ya kutangaza biashara zenu na bidhaa mnazokuwa nazo ndugu zangu biashara ni matangazo msikae kimya,ukizingatia hii ni kampuni ya kitanzania,tuache kukuza vya watu tutukuze vya kwetu ndugu zangu "alisema meya.

"Mnapoona kampuni kama hii ya matangazo ndiyo fursa yenyewe hii ya kuitumia kuzitangaza biashara zenu,ukikaa kimya hakuna mtu anayeweza kuifahamu bidhaa yako au biashara yako hata kama unauza vitu vizuri kiasi gani" alisema Meya.

Kwa pande wake mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company ltd ,Bi. Mary Mollel amesema kuwa kampuni hiyo inapokea matangazo ya aina mbalimbali na Kuyasimamia kwa ukaribu na kwa bei ambayo mteja atakayoimudu.

Hivyo amewataka wafanyabiashara biashara mbalimbali kutokuwa waoga kutangaza biashara zao kwani ndiyo njia pekee itakayowasaidia biashara zao kufahamika zaidi na kupata wateja zaidi.

"Msiwe waoga kuthubutu kutangaza biashara zenu hapa tunasaidiana wewe unaleta tangazo nakutangazia kwa bei nzuri na wakati huohuo unapata wateja kwa upande wako ,kwa maana nyingine tunawezeshana karibuni sana. " alisisitiza Bi Mary. 


Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Airtel yazindua Huduma za Mawasiliano Lindi Vijijini

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akielezea huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa kijiji cha Cheleweni kwa  Mkuu wa wilaya Lindi,  Shaibu Ndemanga (wa pili kulia), baada ya kuzindua mnara huo. Katikati ni Meneja wa Airtel Lindi, Saleh Safy.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
·  Mtandao wa Airtel kutumika kuhimiza elimu ili wazazi kuandikisha watoto Lindi vijijini
LINDI
KATIKA juhudu za kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia maeneo ya pembezoni mwa nchi, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wake wa mawalisiliano na kuanzisha hduma za simu kwa mara ya kwanza katika kijiji cha cheleweni mkoa wa Lindi.

Huduma hizi mpya za mawasiliano zitawafikia wakazia wa vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo kwa kuwahakikishia wakazi wote wa Lindi vijijini huduma za mawasiliano za uhakika, huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na hatimae kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema “ tunayofuraha kupata huduma za mawasilino hapa cheleweni na vijiji vya jirani.  Airtel kwa kuzindua mnara huu, serikali tunaungano jitiada hizi za kuboresha mawasiliano huku vijiji kwa sasa wakazi wa vijiji hivi mtaweza kutumia huduma ya mawasiliano kwa kufany a biashara zenu za nazi kwa kujitafutia masoko sehemu nyingine lakini pia itasaidia kuondoa tatizo lakutembe na fedha nyingi pale mnapofanya biashara kwa kuwa mtatumia huduma za kifedha za Airtel Money kujichukulia fedha zenu wakati wowote


Mkuu wa wilaya aliongeza kwa kusema “Mawasiliano haya yatasaidia sana wilaya yangu katika kukuza elimu kwa kuwa nitaweza kuwawasiliana na watendaji wangu wote wakati wowote. Sasa nitoe tamko kwamba nimeongea na Airtel ili kutuma ujumbe wa meseji kwa wazazi wote kwa kuwa ndio mtandao unaotumika na wengi hapa katika vijiji vyetu vya ng’apa ng’apa  kuhusu kuandikisha watoto wote waliomaliza shule za msingi waende sekondari,  Airtel wamenikubalia sasa ikiwa  mzazi atakaidi kuitikia wito nitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfunga”.

Nataka kuona  huduma hii ya Mtandao wa Airtel tunayoizindua leo inaleta tija katika shughuli za uchumi kama vile uzalishaji wa korosho, kusaidia biashara ndogo za kati na kubadilisha maisha ya jamii kwa ujumla.  Napenda kuchukua fursa hii  kuwahasa wakazi pia kuilinda miundombinu ya mawasiliano haya ili yaduma. Alimalizia kusema Mh,  ……

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel, Saleh Saphy “Tunayofuraha kutoa huduma za uhakika na gharama nafuu nchi nzima, kwa wakazi wa Lindi , tunawahakikishia ofa kabambe za msimu huu wa sikukuu kupitia ofa yetu maalumu ya “Wadatishe” ambayo mnaweza kupata simu orijino kwa gharama nafuu hadi ya shilingi 79,000 tu.-. vilevile wateja wanaweza kupata vifurushi vya intaneti vya 1G kwa shilingi 1000 wakati huu wa msimu wa sikukuu .

Kupitia huduma ya mawasiliano wateja wataunganishwa na huduma za intaneti, huduma za kifedha za Airtel Money kutuma na kupokea pesa, kupiga simu wakati wowote, kusajili simu zao na pia kupata nafasi ya kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao. Hizi ni baadhi tu za huduma zetu hivyo natoa wito kwa wakazi wa cheleweni, Ng’apa na Michee kujiunga na timu ya  Airtel SIBANDUKI na kufurahis huduma zetu.” Alisisitiza Saphy. 

UN NA EU YAWANOA MABALOZI 50 WA MALENGO YA DUNIA IRINGA

UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions). Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akimkabidhi cheti Rais wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa Athman Waziri aliyehitimu kuwa balozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champion).
Picha juu na chini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na zoezi la kutunuku vyeti kwa mabalozi wa malengo ya dunia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champions) baada ya kuhitimisha semina maalum iliyoshirikisha vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Muazarau Matola
Baadhi ya Global Goals Champions katika picha ya kumbukumbu na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na wahitimu wa semina malengo ya dunia (Global Goals Champions) mara baada ya kuhitimisha semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa ambapo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

TIMU YA BUNGE YATUA TANGA KUJIFUA NA MASHINDANO YA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

 Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza akizungumzia maandalizi ya timu ya Bunge kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Kenya.
 Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hotel ya Tanga Beach Resort ambapo timu ya Bunge imeweka kambi.

 Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza katika akiteta jambo na wachezaji wa timu ya Bunge kushoto aliyevaa tisheti nyekundu ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
TIMU ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Bunge Sports Club”imetua mkoani Tanga leo kuweka kambi ya siku tatu kwa ajili ya kujiandaa na Mashindano ya Bunge la Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 14 mwaka huu mjini Mombasa nchini Kenya.

Kikosi cha timu ya Bunge kilichosheheni wachezaji wa michezo ya mpira wa miguu,wavu,riadhaa ,kuvuta kamba na mchezo wa gofu ambao inajumuisha wachezaji 60 ambao watashiriki kwenye mashindanio hayo yanayotazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila kuonekana kujipanga imara.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga mara baada ya timu hiyo kutua,Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza alisema kuwa maandalizi kwa upande wa timu yao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Alisema kutokana na umuhimu wa mashindano hayo waliamua kuweka kambi mkoani Tanga ili kuendana na hali ya hewa kabla ya kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mpango wa kuimarisha kikosi chao.

  “Mimi nisema tu sisi kama timu ya Bunge nia na lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo na ndio maana tumeamua kuweka kambi mkoani Tanga lakini pia hata hivyo pia kikosi chetu kimeimarika kutokana na usajili ambao tumekuwa tukiufanya kila baada ya miaka mitano “Alisema Ngeleja.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Alisema timu hiyo ipo kwenye mazingira mazuri ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo ili kuweza kutimiza dhamira yao waliojiwekea  ya kutwaa ubingwa.
Kwa upande wake,Nahodha wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutimiza dhamira waliojiwekea ya kuibuka na Ubingwa.

  “Nisema tu sisi kama timu ya mpira wa Pete ya Bunge tumejipanga vizuri na kikosi chetu kina hari kubwa ya kuhakikisha tunaiwakilisha nchi yetu ya Tanzania ipasavyo kwa mafanikio makubwa”Alisema. habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

ESRF YAFANIKISHA MKUTANO WA 5 WA MWAKA, WAJADILI UCHUMI

Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Philemon Luhanjo katika mkutano wa siku moja wa kujadili sera za kijamii zinavyoweza kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania, mkutano ambao uliandaliwa na ESRF.

Luhanjo alisema ni vyema Serikali inapokuwa inatunga sera ihakikishe zinakuwa na faida kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kupata maendeleo na kuboresha maisha yao na hata wakati nchi ikielekea katika uchumi wa kati kila mwananchi ahusike na mabadiliko hayo.

"Sera zipo nyingi, zipo za maendeleo ya jumla, elimu, afya, kilimo, viwanda na kila kitu, sisi tunajaribu kuangalia tunapotengeneza sera mbalimbali tuhakikishe kwamba sera hizo zitamnufaisha binadamu, kwamba chochote unachofanya kiwe nikwa faida ya mwanadamu, mipango na malengo yote yawe yanamlenga binadamu kuondoa matatizo yake,

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)

"Serikali inapofanya mipango inatakiwa kupanga mipango ambayo inajaribu kujibu kero za mwananchi, kama ni elimu, kama ni afyaa au kama ni kilimo cha kisasa, tunapotengeneza sera tuwe tunauwianisha, hizo sera zikitekelezeka na mteja wa bidhaa awe ameandaliwa ili mkulima asiwe amepoteza nguvu bure," alisema Luhanjo na kuongeza.

"Tunazungumzia nchi ya viwanda, viwanda gani? na nchi yetu niya kilimo kwahiyo tunatarajia viwanda vingi vitakuwa ni vya kilimo, kwahiyo tunataraji mkulima mdogo aimalishwe ili aweze kuzalisha mazao yanayokwenda kiwandani ni lazima sera ziwe na uwiano mzuri."

Nae Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali inafahamu kuwa nchi haiwezi kupiga hatua bila kuhusisha mwananchi mmoja mmoja na inachofanya kwa sasa na kuwashawishi watu wenye viwanda kutumia malighafi ambazo zinazalishwa nchini ili wakulima nchini wafaidike na uwepo wa viwanda nchini.

"Tunaamini hatuwezi kuwa na uchumi unaokua kama hali ya kijamii ya wananchi haikui na hata Rais Magufuli alikuwa akisema tangu akiwa katika kampeni kwamba Tanzania ya Magufuli niya viwanda, na viwanda hivi ni kwa ajili ya watu wetu,

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.

"Kwenye mpango wetu wa miaka mitano tumesisitiza maendeleo ya viwanda lakini vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini katika kilimo chetu, kwahiyo hatuwezi kuwa na viwanda kama kilimo hakijaendelea, hatuwezi kuwa maendelo ya kijamii kama kilimo chetu hakijaendelea, kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, kwahiyo tumejadili hilo ili kuona wananchi wetu wananufaika vipi," alisema Kijaji. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alizungumza kuhusu mkutano huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kusema,"ESRF kwasasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017, "Katika hiyo ripoti tumeweza kutaharisha ripoti 11 ambazo zitachangia katika utayarishishaji wa hiyo ripoti na dhumuni kubwa ni kuweza kuzijadili hizo ripoti na kupata uelewa mpana ni kwa kiasi gani sera za kijamii zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa Tanzania."
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF, na mashauri wa ufundi wa mradi wa THDR Profesa Marc Wuyts, akiwasilisha mada Situating social policy transformation: A conceptual framework, kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Mhadhiri wa Masuala ya Afrika na Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Shule ya Sayansi ya Siasa nchini Uingereza Dk.Hazel Gray, akiwasilisha mada yake kuhusu mabadiliko katika sera za kijamii kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF.
Mchokoza mada kutoka taasisi ya Daima na Mtafiti mwandamizi mshiriki ESRF, Profesa Samwel Wangwe, akitoa maelezo yake kuhusu mada iliyowasilishwa mezani kwa wajumbe.
Profesa wa uchumi DoE, Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Mushi, akiwasilisha mada kuhusu historia ya sera ya jamii katika mkutano huo.
Mgeni rasmi Dk. Kijaji, (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida, (wa kwanza kushoto), Bi Anna, na mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya ESRF, Bw Philemon Luhanjo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha (wa pili kulia) wakipongeza wakati wa mkutano huo.
Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali kwa makini katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania
Picha ya pamoja ya washiriki, wakuu ESRF, wakiwa na mgeni wa heshima Dk. Kijaji.