Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson
Mmbando (kushoto), akielezea huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel
uliojengwa kijiji cha Cheleweni kwa Mkuu wa wilaya Lindi, Shaibu
Ndemanga (wa pili kulia), baada ya kuzindua mnara huo. Katikati ni Meneja wa
Airtel Lindi, Saleh Safy.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Mtandao wa Airtel
kutumika kuhimiza elimu ili wazazi kuandikisha watoto Lindi vijijini
LINDI
KATIKA juhudu za kuhakikisha huduma za
mawasiliano zinawafikia maeneo ya pembezoni mwa nchi, kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wake wa mawalisiliano na kuanzisha hduma
za simu kwa mara ya kwanza katika kijiji cha cheleweni mkoa wa Lindi.
Huduma hizi mpya za mawasiliano
zitawafikia wakazia wa vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya,
Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo kwa kuwahakikishia wakazi
wote wa Lindi vijijini huduma za mawasiliano za uhakika, huduma za kifedha kwa
njia ya mtandao Airtel Money na hatimae kuendesha shughuli zao za kila siku
kiuchumi na kijamii
Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa
wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema “ tunayofuraha kupata huduma za
mawasilino hapa cheleweni na vijiji vya jirani. Airtel kwa kuzindua mnara
huu, serikali tunaungano jitiada hizi za kuboresha mawasiliano huku vijiji kwa
sasa wakazi wa vijiji hivi mtaweza kutumia huduma ya mawasiliano kwa kufany a
biashara zenu za nazi kwa kujitafutia masoko sehemu nyingine lakini pia
itasaidia kuondoa tatizo lakutembe na fedha nyingi pale mnapofanya biashara kwa
kuwa mtatumia huduma za kifedha za Airtel Money kujichukulia fedha zenu wakati
wowote
Mkuu wa wilaya aliongeza kwa kusema
“Mawasiliano haya yatasaidia sana wilaya yangu katika kukuza elimu kwa kuwa
nitaweza kuwawasiliana na watendaji wangu wote wakati wowote. Sasa nitoe tamko
kwamba nimeongea na Airtel ili kutuma ujumbe wa meseji kwa wazazi wote kwa kuwa
ndio mtandao unaotumika na wengi hapa katika vijiji vyetu vya ng’apa ng’apa
kuhusu kuandikisha watoto wote waliomaliza shule za msingi waende
sekondari, Airtel wamenikubalia sasa ikiwa mzazi atakaidi kuitikia
wito nitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfunga”.
Nataka kuona huduma hii ya
Mtandao wa Airtel tunayoizindua leo inaleta tija katika shughuli za uchumi kama
vile uzalishaji wa korosho, kusaidia biashara ndogo za kati na kubadilisha
maisha ya jamii kwa ujumla. Napenda kuchukua fursa hii kuwahasa
wakazi pia kuilinda miundombinu ya mawasiliano haya ili yaduma. Alimalizia
kusema Mh, ……
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel,
Saleh Saphy “Tunayofuraha kutoa huduma za uhakika na gharama nafuu nchi nzima,
kwa wakazi wa Lindi , tunawahakikishia ofa kabambe za msimu huu wa sikukuu
kupitia ofa yetu maalumu ya “Wadatishe” ambayo mnaweza kupata simu orijino kwa
gharama nafuu hadi ya shilingi 79,000 tu.-. vilevile wateja wanaweza kupata
vifurushi vya intaneti vya 1G kwa shilingi 1000 wakati huu wa msimu wa sikukuu
.
Kupitia huduma ya mawasiliano wateja
wataunganishwa na huduma za intaneti, huduma za kifedha za Airtel Money kutuma
na kupokea pesa, kupiga simu wakati wowote, kusajili simu zao na pia kupata
nafasi ya kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao. Hizi ni baadhi tu
za huduma zetu hivyo natoa wito kwa wakazi wa cheleweni, Ng’apa na Michee
kujiunga na timu ya Airtel SIBANDUKI na kufurahis huduma zetu.”
Alisisitiza Saphy.
No comments:
Post a Comment