Meneja Mawasiliano na Nembo wa Airtel, Arnold Madale (kulia) pamoja na Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto)na Meneja wa huduma za Intaneti,
Erick Daniel wakionyesha bango la offa mpya ijulikanayo kama “Wadatishe””
itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata ofa kambambe ya
Intaneti pamoja na vifaa nafuu vinayotumia intaneti kwa gharama
nafuu zaidi wakati huu wa msimu wa sikukuu
Xxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
leo imezindua Kampeni ya “Wadatishe Intaneti” yenye OFA kabambe maalum
kwa wateja wake nchi nzima ili waweze kufurahia huduma bora za Intaneti pamoja
na kujipatia vifaa nafuu vinayotumia intaneti kwa matumizi binafsi au kwa
kuwanunulia zawadi ndugu jamaa na marafiki katika msimu huu wa sikukuu
Akiongea wakati wa Uzinduzi Wadatishe Intaneti
OFA Meneja wa huduma za Intaneti Bw, Erick Daniel alisema “Wadaitishe
Intaneti” ni ofa ya kipekee kwa kuwa inatoa uhuru kwa kila mteja
kujichagulia kifurushi nafuu kinachoendana na kifaa anachotumia. Vipo vifurushi
vya “Wadatishe Intaneti kwa siku, Wiki au Mwezi vya gharama nufaa ya hadi
shilingi 500 kwa kupiga *149*99# na kuchagua Yatosha Intaneti. Vilevile mteja ataweza kujichangulia Wadatishe
intaneti OFA nyingine kabambe kwa kupitia huduma ya Airtel Money kwa
kupiga *150*60# na kuchagua ofa kabambe kisha Wadatishe
Intaneti ambapo kwa shilingi
1000 tu utapata GB 1 ya intaneti na kwa shilingi 2000 tu pia utaweza kupata GB
2.5 papo hapo na kuanza kufurahia intaneti bora ya Airtel”
Kwa kuongezea, Mteja yeyote ukienda na kununua
kifaa chochote kinachotumia intanent kama vile simu za smartiphone, Modem za
maajabu wingle, au home Wi-FI katika duka lolote la Airtel nchini utafaidi pia
ofa ya punguzo bei la hadi shilling 79,000 na utaunganishwa na OFA ya intaneti
kwa miezi 6 kuanzia sasa” alisema Erick
Kwa Upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Bw,
Jackson Mmbando
alisema “Airtel tunaendelea na dhamira yetu
ya kuhudumia wateja wetu kwa kuwapa kipaumbele kwa kila huduma yetu, hii ndio
sababu kubwa inayotufanya tuwape wateja wetu nchini Uhuru mkubwa wa
kujichagulia, kuanzia leo kupitia ofa za ‘Wadatishe intaneti’ tunaamini
zitatoa unafuu mkubwa kwa kuwaunganisha ndugu, rafiki, na
familia kuwasiliana katika msimu huu wa sikukuu”
Ofa zetu mwaka huu zinatoa punguzo kubwa sana kwa
vifaa vinavyotumia Intaneti kama vile Home Wi-Fi sasa utaipata kwa
shilingi 79,000 tu badala ya shilingi 200,000 na utapewa Home Wi-Fi yako hiyo
ikiwa na kifurushi cha GB 40 BURE. Kwa watakaonunua simu
kama Magnus Z11 itaipata kwa shilling 79,000 tu ikiwa na ofa ya GB 12 kwa muda
wa miezi 6. Vilevile kwa kupitia ushirika wetu na wadau wetu Techno na Huawei katika maduka yetu simu zao zote zitauzwa kwa bei za
punguzo nafuu zaidi ya ilivyozoeleka. Pia ili kukuongeze furaha kwa ofa
tunazotoa kwa watumiaji wa Airtel msimu huu wa sikukuu utafaidi pia ofa
mbalimbali za SMS za bure au muda wa maongezi wa ndani na nje ya mtandao”
alieleza Nchunda
Tunawahimiza wateja wetu kutembelea maduka yetu
yote ya Airtel nchi nzima ili kujinunulia vifaa origino vya intaneti na
kujiunganisha na huduma yetu bora kabisa ya Intaneti kwa kupiga *149*99#
na kuchagua Yatosha Intaneti ili kufurahia Wadatishe Intaneti Ofa” alimalizia
kwa Kusema Bw, Mmbando
No comments:
Post a Comment